SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeiandikia barua
Azam FC ili kupata vielelezo vya rushwa walizopokea wachezaji wao, Deogratius
Munishi ‘Dida’ Aggrey Morris, Said Morad na Erasto Nyoni kama ilivyodai ili
liweze kulifikisha suala hilo katika Kamati ya
Nidhamu.
Angetile Osiah ambaye ni Katibu Mkuu wa TFF, alisema
mara baada ya kupata barua ya Azam ya kuwasimamisha wachezaji wake hao wanne,
waliamua kuijibu kwa kuwataka wawasilishe vielelezo vya tuhuma hizo ili
wavipeleke kwenye Kamati ya Nidhamu.
“Tumewaandikia barua Azam ya kuwataka watuletee
vielelezo walivyotumia kuwakamata wachezaji hao. Kwa sasa tunasubiri vielelezo
hivyo ili kamati iweze kupitia na kujua nini cha kufanya kuhusiana na suala hilo
kwa lengo la kuboresha soka letu,” alisema
Angetile.
Wiki iliyopita
Azam FC iliwasimamisha wachezaji wake wanne kutokana na tuhuma hizo za rushwa
ambapo inadaiwa walipokea kabla ya mchezo dhidi ya Simba ambao uliisha kwa
kikosi chao kufungwa mabao 3-1.
Post a Comment