1.0 Utangulizi
Mtihani wa Taifa wa Kidato
cha Pili mwaka 2012 unatarajiwa kufanyika nchini kote kuanzia tarehe 05/11/2012
na kumalizika tarehe 16/11/2012. Idadi ya shule/vituo vilivyosajili watahiniwa
mwaka 2012 ni 4,242 ikiwa ni ongezeko la vituo 55 ikilinganishwa na vile
vilivyosajiliwa mwaka 2011 ambavyo vilikuwa 4,187. Kwa hiyo kwa mwaka huu kuna
ongezeko la asilimia 1.3.
2.0 Watahiniwa
Jumla ya watahiniwa 442,925
wamejiandikisha kufanya mtihani. Kati yao wasichana ni 214,325 (sawa na asilimia
48.39) na wavulana ni 228,600 (sawa na asilimia 51.61).
3.0 Umuhimu wa Mtihani wa
Kidato cha Pili
Mtihani wa Kidato cha Pili
kama ilivyo mitihani mingine ya taifa ni muhimu sana. Matokeo ya mtihani huu
hutumiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania kama sehemu ya matokeo katika mtihani
wa taifa wa elimu ya sekondari kidato cha nne. Mwaka huu, 2012 matokeo ya
mtihani huu pia yatatumika kama kigezo cha kuchuja na kukariri kidato cha pili
kwa watahiniwa watakaoshindwa kufikia wastani wa ufaulu wa alama
30.
Aidha, mtahiniwa
ataruhusiwa kukariri Kidato cha pili mara moja tu na endapo mtahiniwa atashindwa
mtihani kwa mara ya pili kwa mwaka utakaofuatia, itabidi aendelee na elimu ya
sekondari nje ya mfumo rasmi.
4.0 Hitimisho
Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi inaagiza Wadau wote wa Elimu katika Kanda, Manispaa na Halmashauri za
Wilaya pamoja na Wazazi kuhakikisha kuwa wanafunzi wote walioandikishwa kufanya
mtihani wanafanya bila kukosa.
Aidha, Wazazi, Walezi,
Walimu na jamii kwa ujumla wanashauriwa kuwaandaa vema wanafunzi ili kuepukana
na udanganyifu ikiwa ni pamoja na kuzingatia taratibu na sheria za uendeshaji wa
mitihani.
Nawatakia watahiniwa wote
wa Kidato cha pili mwaka huu mafanikio mema katika mitihani
yao.
Dkt. Shukuru Jumanne
Kawambwa (Mb)
Waziri wa Elimu na Mafunzo
ya Ufundi
04/11/2012

Post a Comment