Na
Waaandishi wetu , hudumabongo@gmail.com
Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi, Tigo imeshikilia usukani wa
biashara inayoongoza kwa kero kwa wateja baada ya kuibuka kuwa mshindi miongoni
mwa biashara 31 zenye kero kwa wateja nchini .
Taarifa hii ni matokeo ya zoezi linaloendeshwa na watumiaji wa mitandao
ya kijamii ya Twitter na Facebook wenye lengo la kuboresha sekta binfasi nchini
Tanzania hususani huduma kwa wateja.
Nafasi ya pili inashikiliwa na Shirika la ugavi wa umeme nchini TANESCO
mkoa wa Dar es Salaam ambao katika mzunguko wa kwanza ndiyo walishikilia usukani
wa kero. Wakiongoza kwa kero ya kukata umeme bila taarifa kitu kinadaiwa kuwa ni
mgao.
Nafasi ya tatu imeendelea kushikiliwa na Kampuni ya mawasiliano ya simu
za mkononi ya Vodacom ambayo imeendelea kushika nafasi hiyo katika mzunguko wa
pili.
Hakukuwa na mabadiliko katika makundi mengine mfano huduma za usafiri wa
anga ambapo mshindi amebakia kuwa ni Precision Air, huku katika huduma za
kibenki zikiendelea kushikiliwa na benki ya CRDB.
Huduma za ving’amuzi vya kulipia vyenye kero imeendelea kushikiliwa na
Star Times waliopata kura 4 za ziada ukilinganisha na matokeo ya
mzunguko wa kwanza.
Katika mzunguko huu biashara mbili zaidi ziliingia katika kinyanganyiro
hicho ambao ni Kampuni mpya ya huduma za ndege ya Fast Jet na Dalalada
inayofanya safari kati ya Mwenge na Kariakoo yenye nambari za usajili T 868
BHU.
Haya ni maoni ya wateja wa huduma hizi yaliyokusanywa kupitia akaunti ya
twitter @hudumambayatz na Facebook group ya HUDUMA BONGO ambapo
jumla ya kero 174 ziliwasilishwa na wateja toka mchuano
uanze.
Zoezi la kukusanya maoni haya linaendelea katika mzunguko wa tatu ambapo
kauli mbiu ya ni “Sisi ndio waajiri wenu , huduma bora ni haki yetu”. Kero
katika huduma na bidhaa mbalimbali za kulipia mfano afya, elimu, usafiri, benki,
mawasiliano zinapokelewa na kutafutiwa suluhisho kwa maendeleo ya taifa
letu.
Kwa
maelezo zaidi juu ya utaratibu wa kura na zoezi hili linavyofanyika tembelea
link ifuatayo http://bit.ly/10SARH1
Post a Comment