MBIO za kuelekea ikulu ya White House nchini
Marekani zimeingia katika
saa za mwisho huku wagombea wakiizunguka nchi
kutoa hoja za mwisho
kuhusu uchumi, uokozi wa viwanda vya magari na
msongamano jijini
Washington.
Obama mwenye umri wa miaka 51 na mpinzani wake
Mitt Romney mwenye
umri wa miaka 65 wanazidiana kidogo kwa mujibu
wa maoni yanayochapichwa
na vyombo vya habari, na kila moja anapambana
kuwashawishi wapiga
kura ambao bado hawajaamua nani
wamchague.
Walipishana jimboni Ohio Jumapili, ambalo ndilo
linalosemakana kuwa
muhimu zaidi miongoni mwa majimbo saba yenye
maamuzi katika uchaguzi
wa Marekani.
Juu ya hilo, Obama alizitembelea New Hampshire,
Florida na Colorado
siku hiyo ya Jumapili, wakati Romney
alizitembelea Iowa, Virginia na
Pennslyvania.
Msisitizo wa Obama katika kipindi hiki ni kwa
wapiga kura kuchagua kati
ya dira mbili.
"Huu siyo tu uchaguzi kati ya wagombea wawili au
vyama viwili, ni
uchaguzi kati ya dira mbili tofatu za
Marekani," alisema Obama.
Rais Barack Obama akitambulishwa na rais wa
zamani Bill Clinton katika mkutano wa kampeni mjini Concord,
New Hampshire.
Hoja za mwisho za Obama jimboni Ohio zilijikita
katika uokozi wa kampuni
za magari za Chrysler na General Motors mwaka
2009, ambao Romney
aliupinga akiwa gavana wa jimbo la Massachusets
wakati huo na kisema
sekta ya magari ilipaswa kuachwa ifilisike.
Matamshi hayo yamekuja
kumuathiri, hasa katika jimbo lenye viwanda
vingi la Ohio.
Katika mkutano siku ya Ijumaa mjini Springfield,
Ohio, Obama aliwaambia
wafuasi wake waliyozomea alipotaja jina la
Romney, kwamba kupiga ndiyo
kisasi bora zaidi.
Romney alitumia mkutano wake mjini Cleveland
kumshambulia Obama
kuhusiana na kauli yake hiyo, na kusema badala
yake, yeye anawaomba
wapiga kura wachague kwa mapenzi ya nchi yao.
Romney alisema
mabadiliko aliyoahidi Obama
yameshindikana.
"Mabadiliko hayawezi kupimwa kupitia hotuba,
mabadiliko yanapimwa
kupitia mafanikio, na miaka minne iliyopita
mgombea Obama aliahidi
mambo mengi kwa watu wengi lakini ametimiza
kidogo sana," alisema
Romney.
Wapambe
wapishana kushawishi wapiga kura
Makundi yanayojitolea kwa ajili ya wagombea
yalikuwa yanapishana katika
majimbo yenye maamuzi, wakiwasiliana na wafuasi
wao kuhakikisha kuwa
watapiga kura na kujitolea kuwasafirisha kwenda
kwenye vituo vya
kupigia kura.
Wakati Romney akiwasihi wafuasi wake waende kwa
wingi katika vituo
vya kupigia kura siku ya jumanne, Obama
anaelekeza juhudi zaidi katika
majimbo yenye maamuzi.
Maoni yamekuwa yakiwaonyesha wawili hao
wakikaribiana kwa sana
lakini wachambuzi wa masuala ya kisiasa
wanasema Obama bado ana nafasi ya kushinda.
Edward Wycof William, mchambuzi wa masuala ya
kisiasa anasema maoni
yamekuwa yakibadilika kutoka wiki moja hadi
nyingine, lakini
kilichoonekana ni kwamba Romney hajaongoza
kabisaa katika maoni
yoyote katika majimbo muhimu.
Mitt Romney akiweka sahihi yake katika fulana ya
mfuasi wake mjini Des Moines, Iowa Novemba 4.
Obama
akumbushia hali ngumu aliyoikuta mwaka 2008
Obama anatafuta awamu ya pili huku kiwango cha
ukosefu wa ajira kikiwa
asilimia 7.2.
Hakuna rais aliyefanikiwa kupata muhula wa pili
tangu kumalizika kwa vita
vikuu vya pili vya dunia kukiwa na kiwango cha
ukosefun wa ajira kilicho
juu ya asilimia 7.2.
Uchumi bado unakua kwa chini ya asilimia 2,
lakini Obama amewakumbusha
wapiga kura juu ya mazingira ya mgogoro
alimochaguliwa miaka minne
iliyopita.
"Kumbukeni mwaka 2008 tulikuwa katikati ya
mgogoro mbaya zaidi tangu
mdororo mkubwa wa uchumi. Tulikuwa katikati ya
vita viwili.
Na sasa biashara zetu zimetengeneza ajira karibu
milioni 5.5, viwanda
vya magari vinafanya vizuri na sekta ya nyumba
inaanza kurejesha thamani
yake, tunategemea mafuta kutoka nje kwa kiasi
kidogo kuliko wakati
wowote katika kipindi cha miaka 20,"
alimesema.
Obama na kuongeza kuwa vita vya Iraq
vimekwisha, vile vya Afghanistan
vinakaribia mwisho na Osamba bin Laden
aliuawa.
Wanajeshi wa Marekani wakiushusha shehena ya
msaada kwa ajili ya
waathirika wa kimbunga Sandy.
Marekani inakwenda kwenye uchaguzi wakati eneo
la kaskazini mashariki
likikabiliana na madhara ya moja ya tufani
kubwa zaidi katika historia ya
nchi hiyo.
Takriban watu milion 27 wamekwisha piga kura
katika uchaguzi wa mapema.
Zaidi ya milioni 130 walipiga kura mwaka 2008.
Wapiga wanatarajiwa
kuamua hatma ya viti vyote 435 vya Bunge la
wawakilishi ambalo
linatarajiwa kuendelea kudhibitiwa na chama cha
Republicans, na theluthi
moja ya viti vya bunge la Seneti lenye viti 100,
ambako chama cha
Democrats kinatarajiwa kuedeleza udhibiti
mdogo.
Uchaguzi wa mwaka huu unafanyika wakati sehemu
ya kaskazini mashariki inakabiliana na madhara ya kimbunga cha Sandy
kilichoharibu maelfu ya makaazi na kuua watu zaidi ya 100.
Waendesha
kura za maoni wamtabiria ushindi Obama
Obama anaendelea kuwa na faida dhidi ya Romney
katika majimbo yenye maamuzi, ambayo ndiyo yanaamua mshindi wa
urais.
Ili kushinda kiti hicho, mgombea laazima kura
270 za majimbo. Obama anahitaji kujihakikishia kura 243 za majimbo yanayoegemea
chama cha Democrats, wakati Romney anaweza kujihakikishia kura 206, na hii
inamuongezea shinikizo la kutafuta zaidi kura za majimbo yenye
maamuzi.
Tayari mawakili wa kambi zote wanajianda kwa
mpanbano mrefu wa mahakani katika majimbo yenye ushindani mkubwa. Baadi ya
wataalamu wanatarajia vuta nikuvute kama zile za mwaka 2000, zilizochukua wiki
tano kumpa ushindi George W.
Bush. Tayari mvutano umeripotiwa jimboni
Florida, baada ya wapiga kura wanaodhaniwa kuwa wa Democrats kuzuiwa na gavana
wa jimo hilo ambaye ni wa chama cha Republican.
Obama na timu yake wakifuatilia mauaji ya Osama
bin Laden. mauaji hayo yamekuwa moja ya hoja zake za kutaka muhula wa
pili.
Maoni yaliyochapishwa na gazeti la Wall Street
Journal siku ya Jumapili yalimpa Obama asilimia moja zaidi ya Romney kitaifa
akiwa na asilimia 48 dhidi ya 47 za Romney.
Tovuti ya Real Clear Politics ilimpa Obama
uongozi wa asilimia 0.2.
Karibu waendesha kura za maoni wote wamemtabiria
ushindi Obama katika kura za majimbo.
Talking Point Memo imempa Obama kura 303 dhidi
ya 191 za Romney, Fivethirtyeight.com imempa Obama kura 307 dhidi ya 231 za
Romney na Pricneton Election Consortium ilimpa Obama kura 277 dhidi ya 206 za

Post a Comment