|
Kiungo
wa Kenya, Kevin Omondi akimdhibiti mshambuliaji wa Sudan Kusini, Martin Kamis
anayejaribu kuondoka na mpira katika mechi ya Kundi A, Kombe la Mataifa ya
Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge, Uwanja wa Mandela, Namboole,
Kampala, Uganda jioni hii. Kenya ilishinda 2-0 mabao ya David Ochieng dakika ya
24 na Clifton Miheso dakika ya 72. Kenya sasa inaongoza Kundi A kwa wastani wa
mabao, ikiwa na pointi sawa na Uganda na Ethiopia ambazo zinamenyana baadaye
kidogo.
|
|
Beki
David Owino akiwatoka wachezaji wa
Sudan
|
|
Kenya
wakishangilia bao la pili
,
|
Kocha
wa timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Mdenmark Kim Polusen
(kulia) akishuhudia kwa makini mchezo wa Kundi A, kati ya Uganda na Ethiopia,
Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Kagame Uwanja wa
Mandela, Namboole, Kampala, Uganda. Wengine kushoto kwake ni Michael Mukunza wa
Executive Solutions, Waratibu wa udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager kwa Stars
na Kocha Msaidizi, Sylvester
Marsh.
|
|
Hatari
kwenywe lango la Ethiopia |
|
Kipa
namba moja wa Uganda, Abbel Dhaira akiwa jukwaani kufuatilia mchezo huo, kushoto
ni kimwana aliyekuwa naye. Abbel hatacheza tena mashindano haya baada ya kuumia
kwenye mechi ya ufunguzi na Kenya jicho lililovimba
kulia.
|
|
Kocha
wa timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Mdenmark Kim Polusen
(kulia) akijadiliana na Msaidizi wake, Sylvester Marsh wakati mchezo
huo.
|
|
on Tuesday, November 27, 2012
Post a Comment