Adam Robert akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu jinsi alivyotekwa na kukatwa viganja vya mikono
Daktari mstaafu wa hospitali
ya mkoa wa Geita, Patrick Bulugu, akionesha kiganja bandia cha mkono wa mtoto
mwenye ulemavu wa ngozi, Adam Robert (13), aliyerejea kutoka nchini Canada jana,
ambako alipatiwa matibabu ya viungo vilivyokatwa kwa imani ya kishirikina. Adam
alipata matibabu kwa msaada wa Shirika la Under the Same
Sun.
DAR ES SALAAM,
Tanzania
MTOTO Adam Robert (13) mwenye
ulemavu wa ngozi jana amerejea nchini akitokea Canada alipokuwa akipatiwa
matibabu ya viungo vilivyokatwa na watu kutokana na imani za
kishirikina.
Mtoto huyo ambaye alifanyiwa
unyama huo mwaka jana akiwa nyumbani kwa wazazi wake ambaye mmoja ni mama wa
kambo 'steps mother' aliweza kusaidiwa na Shirika la Under the Same Sun
linalohudumia watu wenye ulemavu wa ngozi nchini hadi kupata unafuu na kurejea
nchini.
Akizungumza na Waandishi wa
habari, Robert alisema mara baada ya kupatiwa matibabu kwa sasa anajisikia
vizuri na kwamba anaweza kuendelea na shule.
Robert ambaye alikatwa vidole
viwili na nusu ikiwa ni cha gumba na cha shahada huku cha kati kikiwa kimekatwa
nusu alishindwa kuendelea na shule kutokana na kukosa uwezo wa kuandika kwa kuwa
alishindwa hata kushika kalamu.
Kwa mujibu wa Dk.Patrick
Burugo aliyekuwa akimpa matibabu Geita na hatimaye kwenda naye nchini Canada kwa
msaada wa shirika la Under the Same sun alisema matibabu yake yalikuwa makubwa
na ya hali ya juu,mbapo ilimlazimu kutolewa kidole gumba cha mguuni na kuwekwa
mkononi.
Dk. huyo aliyendelea kueleza
kuwa Robert alilazwa katika hospital ya Voncouver ambapo upasuaji wake ulidumu
kwa zaidi ya saa 13 ambapo kuna wakati madaktari bingwa wa upasuaji walilazimika
hata kutoa misuli sehemu nyingine ya mwili na kuunga katika kidole hiko ili
mradi kiweze kupata mawasiliano na kiweze kufanya kazi kwa
haraka.
"Tumefanya upasuaji kwa zaidi
ya saa 13 ambapo ilibidi kidole cha mguu gumba kitolewe mguuni na kiwekwe katika
mkono na kipande cha nyama kukatwa kwenye paja na kuungwa mkononi kwa kweli
matibabu yalikuwa ni ya hali ya juu sana,"alisema
Dk.Burugo.
Hata hivyo mtoto huyo alitoa
ushuhuda wake ambapo alisema hataki kurudi tena nyumbani kwa wazazi wake hao
akihofia maisha yake kuwepo hatarini.
Alielezea tukio zima huku
akieleza kuwa akiwa nyumbani kwao alikuja mgeni ambaye alikaribishwa na mama wa
kambo pamoja na baba yake mzazi ambapo walimtuma kama mara mbili ndani chumvi na
moto.
lieleza kuwa wakati wakiwa
wanamtumna aliweza kufanya kazi zote hzio lakini baada ya kufika kwa muda wa
kulala walimwita atoke nje na ndipo yule mgeni aiyemjua jina kuanza kumkata kata
vidole na sehemu mbalimbali ya mwili.
Alisema wakati akiwa
anafanyiwa vitendo hivyo baba na mama ake walikuwa pembeni lakini yeye katika
kujihami aliamua kum'ngata mtu huyo sehemu zake za siri na ndipo
akamuachia.
"Nilimng'ata sehemu za siri
akaniachia mara moja na ndipo baba akampigia simu baba mkubwa akaja nikapelekwa
hospitali kwa kweli nilipatwa maumivu sana sana,"alisema
Robert.
Naye Mkurugenzi wa Shirika
hilo Vicky Mtekema alisema ni furaha kubwa kwa mtoto Robert kurudi mzima huku
akiwataka watanzania kuacha kufanya vitendo hivyo vya kinyama kwa watu
hao.
Naye Rais na Mwanzilishi wa
shirika hilo Peter Ash aliitaka jamii ya Tanzania kuungana pamoja ili kuweza
kupinga ukatili huo ambao unatokana na imani za kishirikina kwa kisingizio
kwamba wanaweza wakapata madini mengi na kuwa matajiri jambo ambalo si
kweli.


Post a Comment