![]() |
| Mshambuliaji wa Azam, Gaudence Mwaikimba akiwatoka mabeki wa Dragons katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Hisani leo Uwanja wa Martyrs mjini Kinshasa, DRC. Timu hizo zilitoka 1-1. |
Na Mahmoud Zubeiry wa Bin Zubeiry, Kinshasa
WAWAKILISHI
wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, (CAF), Azam FC wameanza
na sare ya 1-1 dhidi ya Dragons ya hapa katika mchezo wa Kundi B kuwania Kombe
la Hisani kwenye Martyrs mjini hapa.
Hadi
mapumziko, wenyeji walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na mshambuliaji
wao hatari, Nkate Jason dakika ya 24.
Nkate
alifunga bao hilo baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Azam, ambao walichanganyana
na kipa wao, Mwadini Ally. Pamoja na kufungwa, Azam walicheza vizuri katika
dakika 45 za kwanza na zaidi walikosa mipango tu ya
kumalizia.
Hata hivyo,
mashambulizi ya pembeni ya wapinzani wao yalilitia misukosuko ya kutosha lango
la Azam katika ngwe hiyo.
Kipindi cha
pili Azam walirudi na kikosi kile kile, lakini walibadilika kiuchezaji na
iliwachukua dakika nne tu kukomboa bao, kupitia kwa Nahodha mpya, Jabir Aziz
aliyeunganisha pasi ya Abdi Kassim ‘Babbi’.
Baada ya bao
hilo, Azam waliendelea kushambulia lango la wapinzani wao, lakini safu ya ulinzi
ya Dragons ilisimama imara kudhibiti mashmbulizi
hayo.
Katika
dakika ya 76, kipa Mwadini alipangua kwa uhodari mkubwa mkwaju wa penalti wa
Mukinzi Mawesi, baaada ya mchezaji huyo huyo kuangushwa kwenye eneo la hatari na
Ibrahim Mwaipopo.
Baada ya
hapo Azam walihamia langoni mwa Dragons, ambao safu yao imara ya ulinzi
iliwanusuru adhabu hii leo.
Azam
ilicheza mechi ya leo bila makocha wake wote wawili, Waingereza Stewart Hall na
Msaidizi wake, Kali Ongala ambao wamebaki Nairobi, Kenya pamoja na Daktari
Mjerumani Paulo Gomez na wachezaji Kipre Balou na Kipre Tcheche kutokana na
kukosa viza za kuingia DRC.
Azam ambao
ni washindi wa pili wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame na
Ligi Kuu, wamepangwa katika Kundi B pamoja na Dragons na Shark FC, ambayo
watacheza nayo Desemba 17.
Ikifuzu
kwenye kundi lake, Azam itaingia Nusu Fainali moja kwa moja, ambazo zitachezwa
Desemba 25 na Desemba 26 itakuwa Fainali na mechi ya kusaka mshindi wa tatu.
Kundi B,
lina timu za DC Motema Pembe, Diables Noirs, FC MK na Real De Kinshasa.
Kikosi cha
Azam leo kilikuwa; Mwadini Ally, Himidi Mao, Waziri Salum, Luckson Kakolaki,
David Mwantika, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Abdi Kassim, Gaudence Mwaikimba,
Abdallah Seif/Humphrey Mieno na Uhuru Suleiman/Zahor Pazi.




Post a Comment