Naibu Waziri wa Wizara ya
Ujenzo Mhe. Eng. Gerson Lwenge akitoa maelezo ya ramani Ujenzi wa Barabara
Ndundu Somanga kwa Mh. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Kipande cha barabara
ambacho ujenzi wake unaendelea kwa kiwango cha lami kati ya Ndundu mkoani Pwani
na Somanga mkoani Lindi chenye urefu wa kilometa 60 sasa umepangwa kukamilika
kabla ya mwezi Juni 2013. Taarifa hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya
Ujenzi Mhe. Eng. Gerson Lwenge wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea mradi huo akitokea mkoani
Lindi.
Mheshimiwa Lwenge
alimjulisha Rais Kikwete kuwa, baada ya mkandarasi huyo kushindwa kuikamilisha
kazi hiyo mwezi Januari 2011 kwa mujibu wa mkataba, taratibu kadhaa zilifuatwa
ili kuhakikisha kuwa mkandarasi huyo anachukuliwa hatua stahiki kwa lengo la
kuhakikisha anaikamilisha kilometa 28 zilizobaki kama
ilivyokusudiwa.
“Hatua kadhaa
zimekwishachukuliwa ambapo kwa sasa mkandarasi ameweza kuongeza uwezo kwa
kuzalisha kilometa 5 za lami kwa mwezi na hivyo kurudisha matumaini kuwa ndani
ya miezi sita kazi hiyo inaweza kuwa imekamilika” alisema Naibu Waziri Injinia
Lwenge..
Mheshimiwa Rais aliitaka
Wizara ya Ujenzi kupitia Tanroads kuhakikisha kuwa inausimamia mradi huo kwa
karibu zaidi ili kuondoa visingizio vingine vyoyote vinayvyoweza kusababisha
mradi huo kuchelewa zaidi.
Ujenzi wa sehemu hiyo ya
barabara ambayo ndiyo pekee iliyobaki katika barabara kuu inayounganisha mikoa
ya Kusini na Jiji la Dar es Salaam, ulianza mwaka 2008 ukiwa umepangwa
kukamilika ndani ya miaka mitatu. Mkadarasi aliyeshinda zabuni hiyo ni Kampuni
ya M/S M.A. Kharafi & Sons kutoka Kuwait kwa gharama ya Shs. 58.8 bilioni.
Fedha hizo zimetolewa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na mifuko ya
maendeleo ya KUWAIT na OPEC.
Post a Comment