Kampuni ya Lakeland Africa ya
jiji Dar es Salaam imeandaa safari ya kutembelea hifadhi za taifa na makumbusho
ya taifa ili kutoa fursa kwa Watanzania kusherehekea msimu huu wa Krismas na
Mwaka mpya.
Watanzania
wanahamasishwa kujitokeza kushiriki katika safari hiyo ya kitalii ya siku 14
itakayoanza jumamosi ya Desemba 14 mwaka huu hadi Desemba 27 mwaka huu. “Kwako
mtanzania sasa inawezekana kujua Tanzania yako, si lazima kuwa mzungu kuwa
mtalii wa ndani”
Safari hii itaanzia Dar es
Salaam, na kupita katika hifadhi za Sadan, Pangani, Lushoto, Tarangire, Ziwa
Manyara, Ngorongoro Crater, Hifadhi ya Serengeti na itahitimishwa Butiama kwa
Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Safari hii itatumia magari ya
kisasa makubwa yenye uwezo wa kubebe watalii 24 na kutoa nafasi kutumia vifaa
vya umeme (laptop, simu, kamera) kwa kila mtalii kuwa na soketi yake. Magari
ambayo yamekuwa yakitumiwa na makampuni ya utalii katika nchi za ulaya sasa
kutumika Tanzania pia.
Gharama za safari hii
zinajumuisha chakula, malazi, usafiri, tozo za kuingia hifadhini na tiketi ya
ndege kutoka Mwanza kurudi Nyumbani.
Kwa mawasiliano na Lakeland
Africa
‘Kuwa mtalii ndani ya nchi
yako’
Post a Comment