Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CANNAVARO, CHOLLO, SELEMBE, AGGREY MORRIS NA MCHA VIALLI WAFUNGIWA KUCHEZA POPOTE DUNIANI

 


Kikosi cha Zanzibar kilichocheza Challenge Uganda

Na Mwandishi Wetu, Zanziabr
NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ni miongoni mwa wachezaji 16, waliofungiwa kwa muda usiojulikana kucheza soka popote duniani na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), ambacho pia kimeivunja rasmi timu ya taifa, Zanzibar Heroes kwa tuhuma ya utovu wa nidhamu.
Akitangaza maamuzi ya kikao cha Kamati Utendaji ya ZFA kilichofanyika leo mchana ofisi za chama hicho zilizopo Kiembe Samaki, nje kidogo ya mji wa Zanzibar, Makamu wa Rais wa ZFA Unguja, Alhaj Haji Ameir, alisema Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji waliohudhuria kikao wameunga mkono hatua hiyo, ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine.
Kikao hicho cha dharura kimekuja kufuatia sakata la wachezaji wa Zanzibar Heroes kuamua kugawana kiasi cha dola za Kimarekani 10,000 walizopata baada ya kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge iliyomalizika wiki iliyopita mjini Kampala, Uganda, kufuatia kuifunga Bara, Kilimanjaro Stars kwa penalti 6-5, baada ya sare ya 1-1.
Inadaiwa kuwa wachezaji hao waliamua kugawana fedha hizo kwa madai kuwa wamekuwa wakidhulumiwa fedha zao na ZFA.
Hata hivyo katika ufafanuzi uliotolewa leo na Katibu Mkuu wa ZFA Taifa, Kassim Haji Salum, amesema haijawahi kutokea wachezaji wa timu hiyo kudhulumiwa haki yao akikumbushia fedha za zawadi walizopata mwaka 1995 katika mashindano kama haya yaliyofanyika nchini Uganda na Zanzibar ikafanikiwa kutwaa ubingwa na mwaka 2009 waliposhika nafasi ya tatu na mara zote walipewa stahili zao.
Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Zanzibar, Salum Bausi ambaye jana alitangaza rasmi kujiuzulu kuifundisha timu hiyo, amesema hatua hiyu ni sahihi kabisa kwa sababu kitendo hicho kimewafedhehesha wadau wa soka na Wazanzibari kwa ujumla.
Tayari ZFA Taifa walikwishatuma barua rasmi kwa TFF juu ya hatua hiyo huku nakala ya barua hizo zikitarajiwa kusambazwa kwa vilabu wanavyochezea wachezaji hao.
Wachezaji wanne walionusurika na adhabu hiyo ni wale walioamua kuzirejesha fedha hizo ambao majina yao hayakutatwa kwa sababu maalum, hata hivyo taarifa zilizopo ni kuwa wachezaji hao wanatoka katika klabu ya Kipanga timu inayomilikiwa na JWTZ, Jamhuri, Zimamoto na KMKM.
Kikosi cha Zanzibar kilichokwenda Challenge ni makipa; Mwadini Ali (Azam), Suleiman Hamad (Black Sella), Abdalla Juma (Kipanga), mabeki; Nassor Masoud 'Chollo' (Simba), Samir Haji Nuhu (Azam), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub Ali 'Canavaro' (Yanga), Aziz Said Ali (Kmkm), Mohammed Juma Azan (JKU) na Ali Mohammed Seif (Mtende Rangers).
Viungo ni; Hamad Mshamata (Chuoni), Ali Bakar (Mtende Rangers), Is-haka Mohammed (JKU), Twaha Mohammed(Mtibwa Sugar), Suleiman Kassim 'Selembe' (Coastal Union), Saad Ali Makame (Zanzibar All Stars), Makame Gozi (Zimamoto), Issa Othman Ali (Miembeni), Aleyuu Saleh (Black Sella), Khamis Mcha Khamis 'Viali' (Azam) na washambuliaji; Amir Hamad (JKT Oljoro), Jaku Juma Jaku (Mafunzo), Abdallah Othman (Jamhuri), Nassor Juma (JKU) na Faki Mwalim (Chipukizi).
 
chanzo: Bin Zubeiry
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top