NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu, amesema serikali kuanzia sasa itawakamata baadhi ya watu waliyojianzishia viwanda bubu vinavyozalisha bidhaa hafifu nchini.
Kauli hiyo ilitolewa, na
waziri huyo wakati alipotembelea viwanda vinavyomilikiwa na Kampuni ya MMI
Steel Mills Limited vilivyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam
jana.
Alisema
lengo la kuwakamata watu hao ambao wamo hata
wageni
,
na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ni kudhibiti bidhaa hizo kwenye soko
ambapo zimekuwa zikiwatia hasara wananchi pia kuviharibia sifa baadhi ya
viwanda.
Teu alisema viwanda hivyo
vimekuwa vikiiga bidhaa kama nondo na mbati, kutumia nembo za kampuni mbalimbali
zinazotambulika nchini kama vile MMI Steel Mills Limited.
Alisema kutokana na
ubabaishaji huo unaofanywa na baadhi ya watu, serikali itahakikisha inazisaidia
kampuni zote zilizoanzishwa kwa kufuata sheria.
“Kampuni hii ya MMI Steel
Mills imekuwa kwa muda mrefu ikitoa mchango mkubwa katika kuchangia pato la
taifa haswa kwenye eneo la kodi pia imepanua wigo wa ajira kwa Watanzania ambapo
pia kimekuwa kikiingizia Tanesco jumla ya sh. bilioni 1 kama bili kwa mwezi
”alisema Teu.
Akizungumzia kuingiliana
kwa mipaka kati ya Kiwanda hicho na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC katika
mradi wa kutengeneza chuma cha Liganga na mkaa wa mawe huko Katewaka, Teu
alisema, hata yeye utata huo umemshtua sana.
Alisema matatizo hayo
yamesababishwa utoaji wa zabuni, kutokana na upande mmoja kutokuwa makini ambapo
pia aliwaomba wasichoke, watalifanyia kazi kama wizara.
Awali Mhandisi, Raulence
Manyama viwanda hivyo vya chuma, vilikuwa vikikabiliwa na changamoto ya
upatikanaji wa chuma.
Alisema hadi kufikia mwa
2012 kulikuwa na viwanda na viwanda 21 vya chuma nchini vyenye uwezo wa
kuzalisha zaidi ya tani 200,000 za chuma kwa mwaka.
Aliasa serikali kuongeza
uwezo nchi kuzalisha aina nyingi ya bidhaa ya chuma ambazo kwa sasa zinatoka
nchi za nje, hizo ni hot-roll coils, cold coils, flat bars na aina nyingi za
chuma.
Post a Comment