Kauli hiyo ya CUF ilitolewa juzi na Katibu Mkuu wake , Maalim Seif Shariff Hamad wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Alabama Miembeni.
Maalim Seif alisema kama Tume hiyo haikuweka bayana muundo wa mabaraza hayo na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinaweza kutumia mwanya huo kuteua wanachama wao ili wapate kulinda sera yao ya muundo wa Muungano uliopo sasa.
“Nasema hivi kwa sababu maraisi wote wawili ni wa CCM kwa hiyo wanaweza kutumia mwanya huu kuteua wafuasi wao ili wapate kutimiza idadi ya wajumbe,” alisema Katibu Mkuu huyo.
Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, alisema itakuwa jambo zuri sana kama wananchi watawekwa wazi katika kuunda mabaraza hayo.
“Naweka wazi kama kama Mabaraza haya yatakuwa na wanachama wa CCM peke yao hatuwezi kukubali abadani,” alisema Hamad.
“Lazima kuwe na uwazi na wananchi waelezwe Mabaraza hayo yataundwa na wajumbe wepi, ili kuondoa dhana mbaya inayoweza kujengwa na wananchi kuwa wajumbe hao watatoka katika chama kimoja cha siasa,” alisema Maalim Seif.Kutokana na dhana hiyo, Maalim seif aliitaka Tume ya Kukusanya maoni ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania kuchukua hadhari mapema juu ya suala hilo ambalo linaweza kuharibu mchakato mzima wa maoni hayo.
Sambamba na hilo Maalim Seif alisema hata katika suala la kura ya maoni itakayokuja kufuatia huko mbele, bado kuna masuala mengine ya kujiuliza, kuhusu utaratiubu upi utatumika, wakati wa kura hiyo kwa Wazanzibari wanaoishi Tanzania Bara na watu wa Tanzania Bara wanaoishi Zanzibar.
Alieleza kuwa hofu hiyo
inakuja kwa vile sheria ya mabadiliko ya katiba inasema mabadiliko hayo
yatapitishwa, iwapo angalau nusu ya wananchi wa kila upande kati ya Tanzania
Bara na Zanzibar wataunga mkono mabadiliko hayo, hivyo amehimiza mambo hayo
lazima kwanza yawekwe wazi.
Post a Comment