Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KAMPUNI YA STARTIMES NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA YA DIGITALI

Kwa maelekezo ya ITU kwamba huduma za televisheni za utangazaji kubadili kutoka Analojia na kwenda katika mfumo wa digitali kabla ya Juni 17, 2015, lakini kwa nchi ya Tanzania tarehe ya mwisho ya kubadili mfumo ni Desemba 31, 2012.
Ili kuwa na uwezo wa kutekeleza mabadiliko haya katika wakati, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) imeunda kampuni ya Ubia na kampuni ya Star Communication Network Technology Co. LTD ya China, inayojulikana kama Star Media (Tanzania) LTD inayotumia jina la kibiashara la STARTIMES. wajibu wa Kampuni hii ya Ubia na ya kisasa, ni kuleta mapinduzi katika huduma za televisheni na utangazaji kwa njia ya digitali na kutoa huduma za multiplex katika Tanzania. STARTIMES tayari imeshabadili na kuingiza katika mifumo ya digitali mikoa saba katika Tanzania Bara yaani Mwanza, Mbeya, Dodoma, Arusha, Moshi, Tanga na Dar es salaam. Kufikia mwisho wa mwaka huu,kabla ya kubadili rasmi mfumo mkoa wa Morogoro pia utaunganishwa katika mfumo wa digitali kama miko tajwa.
Inatarajia pia kujenga Kituo cha kurushia cha kisasa katika eneo la Makongo kilimani ili kuboresha signal/urushwaji wa matangazo yetu katika Mkoa wa Dar es Salaam na baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Pwani.
Kampuni ya Star Time vile vile inakusudia kubadili Zanzibar na tayari tumepata leseni kwa ajili ya kujenga kituo cha televisheni na kupeleka huduma za mfumo wa digitali kabla ya tarehe ya kubadili (Switch –off) kama kila kitu kitakwenda kulingana na mipango yetu. Hata hivyo, mpango wetu ni kwamba Tanzania nzima lazima kubadilishwa kwenda kwenye mfumo wa digitali mapema iwezekanavyo ili kila Mtanzania anaweza kufurahi ulimwengu wa digitali.

Kwa miezi miwili iliyopita STARTIMES ilikua katika maadhimisho ya uzinduzi wa huduma za matangazo ya digitali Tanzania. Wakati wa maadhimisho haya STARTIMES imepunguza bei ya kawaida ya kuuza ving’amuzi vyake kwa 44%, yaani kutoka shilingi 70,000 / = hadi shilingi 39,000 / =. STARTIMES ilipanga kufikia kilele cha maadhimisho haya mnamo Oktoba 15, 2012. Hata hivyo, kutokana na kutangazwa na serikali kwamba Tanzania lazima kubadili mfumo wake kwenda digitali kufikia mwisho wa mwaka huu, STARTIMES imeamua kuendelea kuuza ving’amuzi vyake kwa bei zilizotajwa hapo juu kwenda na maono yetu ambayo ni, kuwezesha kila nyumba kuwa na upatikanaji wa digitali na kumudu kumiliki luninga ya digitali; kuangalia matangazo ya digitali na kufurahia ulimwengu wa digitali.
Katika juhudi hizo za kufanya Watanzania kufurahia michezo duniani kote, STARTIMES sasa inaonyesha michezo inayopedwa zaidi katika mechi za mpira za Ligi Ulaya kwa kupitia DTV. STARTIMES sasa iko katika maadalizi y kwa ajili ya Sikukuu za Krismasi ambapo nia ya kuja na mambo mkubwa kwa ajili ya digital televisheni za 21 “CRT, 24 LCD, 32 LCD na 42 LED na zawadi zaidi kwa wateja wote ambao tayari wanatumia huduma zetu na wateja wapya pia. Kwa habari zaidi tembelea maduka yetu na Ofisi za StarTimes na kwa Mawakala wetu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top