Afisa
Uendeshaji wa Mfuko wa LAPF Kanda ya Mashariki, Emmanuela Meishaa (kushoto)
akifafanua jambo katika Jukwaa la Sanaa wakati alipowasilisha mada ya Umuhimu wa
wasanii na Wadau wa sanaa kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii. Kulia ni Sarah
Mushi, afisa Maendesho wa LAPF.
Katibu Mkuu
wa Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) Hassan Bumbuli,
Akizungumza katika Jukwaa la Sanaa, kushoto ni Maofisa kushoto ni Maofisa kutoka
Mfuko wa Pensheni wa LAPF ambao walizungumzia umuhimu wa Wasanii kujiunga na
Mifuko ya hifadhi ya Jamii.
=======
======== ====== ========
Wasanii
nchini wametakiwa kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika mifumo ya hiari
kwa lengo la kujiwekea akiba ya kuwasaidia katika masuala mbalimbali kwenye
maisha baada ya kufikia hali ya kushindwa kufanya kazi.
Akiwasilisha mada ya umuhimu wa wasanii na wadau
wa sanaa kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Afisa Utekelezaji wa Mfuko wa
Pensheni wa LAPF, Emmanuel Maishaa amesema katika kipindi hiki ambacho
Serikali imetoa uhuru kwa mifuko kusajili wanachama walio nje mifumo rasmi ya
ajira ni vyema wasanii kutumia nafasi hiyo kujiunga na mifuko na kujiwekea
akiba.
“Tunafahamu
kwamba si rahisi pengine msanii kupata fedha kila mwisho wa mwezi, lakini kwa
mfumo wetu LAPF tunatoa nafasi ya kuchangia kadri unavyopata. Nadhani na mifuko
mingine inautaratibu wake lakini LAPF tumeliangalia hilo na kutoa nafasi nzuri
zaidi ili hata msanii mwenye kipato cha chini kabisa aweze kumudu kuchangia,”
alisema.
Amesema kwa
kujiunga na mifuko ya jamii hasa LAPF wasanii wanaweza kupata faida nyingi ikiwa
ni pamoja na kunufaika na mafao mbalimbali yanayotolewa na mifuko hiyo hivyo
kujiwekea mazingira mazuri ya baadaye au ya kuwawesha kufanya mambo yao kwa
urahisi baadaye.
“Msanii
anaweza kujiunga na mfumo wa hiari ambapo baada ya mwaka mmoja LAPF inatoa
nyongeza ya asilimia tano kwenye michango yake, na anaweza kujitoa wakati wowote
baada ya kutimiza mwaka mmoja, katika mfumo huu kiwango cha chini cha
kuchangiakwa mwezi ni shilingi 20,000/- ambapo msanii anaweza kulipa kiwango
hicho kwa awamu na kwamba kuna nafasi ya kulipia kwa mkupuo kama amechelewa au
kupitisha mwezi mmoja,” alisema
Post a Comment