NAFASI ZA
UFADHILI WA MASOMO YA SEKONDARI KWA YATIMA WA KIKE
RafikiElimu
FOUNDATION ni Taasisi isiyokuwa ya kiserikali inayo jishughulisha na
Maendeleo ya jamii. Taasisi inapenda kutangaza nafasi za ufadhili wa
masomo ya sekondari kwa waombaji wenye sifa zifuatazo
:
1. Awe
yatima wa jinsia ya kike au awe masichana anayeishi katika mazingira
magumu.
2.Awe raia
wa Tanzania.
3. Awe
anajiandaa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza kuanzia Januari
2013. AU
4. Awe
anajiandaa kujiunga na masomo ya kidato cha tano katika mwaka wa
masomo 2013/14.
5. Awe ni
mwanafunzi ambaye tayari anasoma sekondari lakini anashindwa/ ama
ameshindwa kuendelea na masomo yake kutokana na kufiwa na wazazi ama
walezi wake.
* N.B :
Ufadhili wa masomo kwa kidato cha tano na sita utatolewa kwa wanao
taka kuchukua masomo nya michepuo ya ARTS.
Tuma barua
yako ya maombi ya ufadhili wa masomo kwenda kwa :
MKURUGENZI
MTENDAJI,
RAFIKIELIMU
FOUNDATION,
S.L.P
35967,
DAR ES
SALAAM.
* Katika
barua yako ambatanisha barua ya serikali ya mtaa unaoishi, cheti chako
cha kuzaliwa ama Hati ya Kiapo " AFFIDAVIT " , picha zako nne za rangi,
pamoja na vielelezo vingine vinavyo thibitisha kwamba wewe ni
yatima.
* Maombi
yako yatufikie kabla ya tarehe 07 JANUARY 2013.
* Maombi
yanaweza kutumwa na msimamizi wa mwanafunzi husika kwa niaba
yake.
Kwa
maelezo zaidi tembelea www. rafikielimu. blogspot.com
Post a Comment