Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Bibi Chiku Galawa akimkaribisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad katika Mkoa huo mara baada ya kuwasili katika
uwanja wa ndege wa Tanga.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimia na vikosi vya
ulinzi na usalama pamoja na wananchi wa Mkoa wa Tanga, mara baada ya kuwasili
katika uwanja wa ndege wa Tanga.
Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimia na wananchi mbali mbali
waliojitokeza kumpokea wakati walipowasili katika uwanja wa ndege wa Tanga kwa
ziara ya siku mbili. (Picha na Salmin Said, OMKR)
Na Hassan Hamad,
Tanga
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema wananchi
wanahitaji kuelimishwa zaidi juu ya uhifadhi wa mazingira ili waweze kuyalinda
na kuepuka kuyachafua.
Amesema
uchafuzi wa mazingira mara nyingi umekuwa ukisababishwa na wananchi wenyewe,
jambo ambalo linapaswa kupigwa vita kwa wananchi kupatiwa elimu ya mazingira ili
kuepusha uharibifu huo.
Maalim
Seif ameeleza hayo wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Tanga bibi Chiku
Galawa, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga kwa ziara ya siku
mbili.
Amesema
iwapo wananchi wataelimishwa ipasavyo wataweza kujiepusha na uharibifu wa
mazingira, ikiwa ni pamoja na kukata miti kiholela bila ya kuzingatia athari za
kimazingira.
Nae
Mkuu wa Mkoa wa Tanga bibi Chiku Galawa amesema uharibifu wa mazingira ni moja
kati ya changamoto kubwa zinazoukabili Mkoa huo, jambo ambalo linarejesha nyuma
maendeleo ya kiuchumi katika Mkoa huo.
Amesema
Serikali ya Mkoa huo inatafuta njia mbadala ya kutumia nishati nyengine ili
kupunguza matumizi ya kuni ambayo yanachangia ukataji wa miti
kiholela.
“Iwapo
serikali itazuia matumizi ya makaa na kuni, serikali na wananchi watapata nafasi
ya kufikiria nishati mbadala ya kutumia kwa ajili ya kupikia, lakini tukiendelea
kutumia kuni mawazo yetu yatabakia hapo hapo tu na tutaendelea kutumia kuni kila
siku”,alitanabahisha bibi Chiku.
Amesema
ukataji wa miti kiholela katika Mkoa huo umekuwa ukichangia kuwepo kwa athari za
mabadiliko ya tabianchi yanayopelekea kuweko kwa upungufu wa mvua pamoja na
kuongezeka kwa hali ya joto.
Hata
hivyo bibi Chiku amesema Mkoa huo umepiga hatua kimaendeleo, ikiwa ni pamoja na
kuimarika kwa miundombinu ya barabara.
Akiwa
Mkoani Tanga, Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF
anatarajiwa kuhutubia mikutano mitatu ya hadhara katika viwanja vya Tangamano,
Kwadiboma Sokoni na Handeni.
Post a Comment