Kikosi cha timu ya Chama Cha waandishi wa habari za
Mizhezo TASWA FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa
kirafiki kati yake na timu ya Bagamoyo Veteran uliofanyika kwenye uwanja wa
Mawanakerenge Mjini Bagamoyo jioni ya leo, ambapo timu ya TASWA FC imechapwa
magoli 4-0 na maveterani hao kutoka mjini Bagamoyo,
Timu ya Waandishi wa habari ya TASWA FC imeshiriki
katika mchezo huo ikiwa ni moja ya programu ya mkutano wa chama hicho
unaotarajiwa kufanyika kesho kwenye hoteli ya Kiromo View mjini Bagamoyo ambapo
utafunguliwa na Ridhiwani Kikwete na Kufungwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari
Maelezo ndugu Assah Mwambene PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.
Kikosi cha timu ya Bagamoyo Veteran kilichotoa
kichapo kwa timu ya TASWA FC mjini Bagamoyo leo.
Baadhi ya waandishi wa habari ambao ni mashabiki wa
timu hiyo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo
huo.
Mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu ya Simba
Ibrahim Masoud katikati akizungumza na Mzee Willy Chiwango kutoka gazeti la This
Day kulia na Beny Kisaka mkurugenzi mwanadamizi gazeti la Jambo
Leo.
Mkuu wa Wilala ya Bagamoyo Ahmed
Kipozi wa pili kutoka kulia akizungumza na mwandishi mkongwe kutoka Zanzibar
Said Salim huku wanahabari wengine wakifuatilia mazungumzo hayo.
Mchezaji wa timu ya TASWA FC Juma Pinto akimiliki
mpira mbele ya beki wa timu ya Bagamoyo Veterani katika mchezo huo uliofanyika
kwenyeuwanja wa Mwanakerenge mjini Bagamoyo
Mchezaji wa timu ya TASWA FC Shafii Dauda akimiliki
mpirahuku beki wa timu ya Bagamoyo Veterani akiuwania katika mchezo huo,
katikati ni mchezji wa timu ya TASWA FC Mohamed Akida.
Mshauri wa timu ya TASWA FC Masoud Sanani akihimiza
wachezaji wa TASWA FC kucheza kwa bidii baada ya kuchapwa magoli 4-0 huku
wachezaji wa timu hiyo wakishangaa wasijue la kufanya wakati zikiwa zimesalia
dakika za majeruhi
Post a Comment