Na: Heka
Wanna na Shakila Galus-MAELEZO_DAR ES SALAAM
ZAIDI ya wanafunzi 300
wa udaktari kutoka nchi mbalimbali duniani wanatarajiwa kufanya mkutano wa
kimataifa utakaojadili jinsi ya kutatua migogoro katika sekta ya Afya kwenye
ukanda wa Afrika.
Hayo yalisemwa na Rais
wa Chama cha Wanafunzi wa Udaktari Tanzania(TAMSA) Francis Tegete wakati
akizungumza na waandiishi wa habari jana jijini Dar es salaam.
Alisema kuwa washiriki
wa mkutano huo watajadiliana jinsi ya kuboresha rasilimali watu ,sera za afya na
miundo mbinu ya kutolea huduma ya afya katika nchi zao ili kutimiza malengo ya
Melinia .
Alisema kauli mbiu ya
mkutano huo inalenga kujadili migogoro ya afya barani na jinsi ya kuitatua kwa
ajili ya kutoa huduma bora kwa wananchi hasa wanaoishi katika mazingira magumu
na vijijini.
Tegete aliongeza kuwa
mkutano huo utakuwa muhimu kwa wanafunzi wa udaktari nchini kupata fursa ya
kubadilishana uzoefu na wenzao wa jinsi gani wanavyoweza kusaidia katika utoaji
wa huduma za afya ikiwemo upunguzaji wa vifo vya watoto na mama
wajawazito.
Alisema kuwa mkutano
huo utafunguliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi siku ya
Jumanne tarehe 18 na kumalizika 22 Disemba mwaka huu jijini
Arusha.
Baadhi ya washiriki
wanatoka Marekani , Uingereza, Lebanon, Sierra Leone , Uganda, Kenya , Rwanda,
Burundi, Congo, Korea Kusini, Sudan, Zambia , Ethiopia na Sweden


Post a Comment