Mbunge wa Jimbo la
Ukonga,Mh. Eugean Mwaiposa (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo
pichani) kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Dar es Salaam mapema leo
asubuhi wakati wa kutangaza uzinduzi wa Mkakati wake wa kuwainua kiuchumi
wananchi wa Jimbo lake la Ukonga kupitia Mradi aliouanzisha ujulikanao kama
"JAMII NA MAENDELEO UKONGA",ambapo amefanikiwa kuvikusanya vikundi vya
wafanyabiashara ndogo ndogo waliopo kwenye Jimbo la Ukonga na kwa umoja huo pia
ameanzisha Saccos ya Jimbo itakayowawezesha wafanyabiashara hao kupata mikopo ya
kuendeleza biashara zao inayotambulika kwa jila la UKONGA VICOBA SACCOS LTD
(UVICOSA).Kulia ni Mwenyekiti wa Muda wa Saccos hiyo,Bi. Adivela
Ruge.
Katibu wa Ukonga Vicoba
Sacos (UVICOSA),Bi. Mary Katobes (kushoto) akiongea wakati wa kuwahamasisha
wananchi wa jimbo la Ukonga (kupitia vyombo vya habari) kujitokeza kwa wingi
kujiunga na Sacos yao hiyo.
Meneja wa Mradi wa Jamii
na Maendeleo Ukonga,Suzan Miseda akiongea katika mkutano huo na Waandishi wa
Habari.
Post a Comment