Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga (wa pili kushoto) akiwasili
katika Hotel ya White Sands jijini Dar es Salaam kujionea jinsi Hoteli hiyo
iliyopo ufukweni mwa bahari inavyotunza mazingira yake. Kulia ni Meneja Mkuu wa
Hoteli ya White Sands Alwyn Kellerman na Afisa Mazingira wa Hoteli hiyo Bi.
Linda Mbuya.
Mmoja wa wafanyakazi wa Hoteli hiyo
akifunua chemba inayopitisha maji taka kwa ajili ya kukaguliwa na jopo la
wataalam kutoka NEMC na Maafisa wa Wizara. Katika ukaguzi huo Naibu Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga hakuridhishwa na
jinsi hoteli hiyo inavyoendesha mfumo wake wa maji taka na kuagiza timu ya
wataalam kutoka NEMC kufanya ukaguzi upya wa mifumo hiyo.
Meneja Mkuu wa Hoteli ya Giraffe
Ocean View Bw. Nicholas Oyieko akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Mh. Kitwanga (wa
pili kushoto) jinsi hoteli hiyo inavyotunza mazingira na namna inavyodhibit
mfumo wake wa maji taka kuhakikisha kwamba haileti madhara.
Hii ni sehemu iliyoko pembeni ya
Hoteli ya Giraffe ambayo mmiliki wake hafahamiki ambayo imewekwa uzio na kufanya
bahari kushindwa kupumua vizuri na kusababisha mkusanyiko wa uchafu unaodaiwa
kutuama mahali hapo tangu mafuriko ya hivi karibuni yaliyoikumba jiji la Dar es
Salaam. Naibu Waziri ameamuru muhusika kutafutwa mara moja na kupigwa faini na
kuamuriwa kuondoa vifusi hivyo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga na ujumbe wake wakiangalia eneo
hilo.
Wataalamu
kutoka NEMC na Maafisa wa Wizara wakikagua moja ya chemba za hoteli hiyo
zilizounganishwa na mabomba yanayochuruzisha maji baharini ambapo Hoteli hiyo
ilidanganya kwa kusema kwamba kila chemba hizo zinapojaa wanaita gari maalum la
kunyonyea maji taka hayo kitu ambacho si kweli kwa mujibu wa watalaam wa
NEMC.
Moja
ya bomba la maji taka kutoka katika hoteli hiyo yanayotiririkia
baharini.
Pichani
ni Matundu ya mabomba ya maji machafu yanayotokea Hoteli ya Double Tree By
Hilton yaliyoelekezwa baharini.
Naibu
Waziri Mh. Charles Kitwanga akitoa amri kwa Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa
Mazingira (Enviromental Impact Assessment-EIA) wa Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw.Ignace Mchallo ambapo ametoa muda wa miezi
miwili kwa uongozi wa Hoteli ya Double Tree kutafuta njia nyingine ya kumwaga
maji taka isiyochafua fukwe na maji ya bahari akisema kuwa yeye si mzungumzaji
sana bali anasimamia vitendo. Mheshimiwa Waziri amemtaka Bwana Mchallo kusimamia
utekelezaji wa zoezi hilo.
Mwanasheria
wa NEMC Bw. Mwanchane Heche akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema
watachukua hatua kuanzia kesho (7 Disemba 2012) kwa kuwa Afya za watu hazisubiri
muda hivyo tunauwezo wa kumfungia biashara yake, kumlipisha faini au vyote kwa
pamoja na tutahakikisha anaacha kumwaga maji taka eneo la
baharini.
Mwanasheria
wa NEMC Bw. Mwanchane Heche akimpa utaratibu wa mamlaka yake hatua itakayochukua
Meneja Mkuu wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Bw. Sven Lippinghof akimweleza
kuwa japokuwa huduma zao ni bora mfumo wao wa maji taka unahatarisha Afya za
Wananchi na kuharibu Mazingira.
Huu
ni muonekano wa Hotel ya Double Tree By Hilton kwa nyuma Upande wa bahari ambako
ndiko wateja wao wanakopumzika na kupunga upepo mwanana wa baharini kunakomwagwa
maji machafu ya kinyesi.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga ( wa pili
kushoto) akizungumza na Meneja Mkuu wa Hoteli ya Coral Beach Hans Heuer
(kushoto) ambako alihitimisha ziara yake.
Mh.
Charles Kitwanga na Ujumbe wake wakikagua miundo mbinu ya eneo la Coral Beach
Hoteli.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga akitoa
maoni yake kwa Uongozi wa NEMC na kusema kuwa ameridhishwa na hali ya mazingira
na utaratibu unaotumiwa na Hoteli hiyo.
Post a Comment