Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Mh. Lazaro Nyalandu akizungumza na waandishi wa habari jijini dare s Salaam leo akifafanua juu ya hatua serikali ilizochukua kufuatia sakata la kampuni ya kitalii ya Ahsante Tours kufungiwa kuingiza wageni TANAPA baada ya kupata maelezo ya kina kutoka kwa wamili wazawa wa kampuni hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu kupitia wizara yake amewasiliana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) ili ifanye uchunguzi dhidi ya tuhuma za kufungiwa kwa kampuni ya kitalii ya Ahsante Tours iliyoko Moshi.
Akifafanua sakata hilo Mh. Nyalandu amesema kampuini hiyo ya kitalii ya Mkoni Kilimanjaro ilifungiwa kuingiza wageni wake katika Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuanzia tarehe 17 November 2012 kutokana na madai ya kuwa na deni wanalodaiwa.
Kwa mujibu wa maelezo ya wamiliki wa kampuni hiyo waliomtembelea waziri ofisini kwake na mazingira ya TANAPA kuchukua hatua ya kuwafungia, ni dhari kuna wafanyakazi ndani ya makao makuu ya TANAPA ambao wanashiriki kulihujumu shirika na kulinda maslahi yao ikiwepo taarifa za rushwa na unyanyasaji wawekezaji wazawa.
Amesema serikali haiwezi kuwavumilia wala kuwaogopa na itawachukulia hatua za kinidhamu na kisheria wale wote watakaobainika kuwa sehemu ya ya huo mtandao wa rushwa na dhuluma dhidi ya wawekezaji wazawa.
Aidha amesema serikali itachukua hatua zaidi dhidi ya Bodi ya Wadhamini kwa kupitia maamuzi ambayo yana athari kwa taifa na yasiyozingatia kuwapa kipaumbele wazawa katika tasnia ya utalii nchini.