Mgeni rasmi katika Sherehe
za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda
akiwasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kusalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe
Poinsot.
Pichani Juu na Chini ni
maandamano ya kuadhimisha siku ya Haki za Binadamu yaliyohusisha Taasisi
mbalimbali za Serikali na zisizo za kiserikali, Wanafunzi wa Shule za Sekondari
na Wanaharakati wa Haki za Binadamu yakiwasili katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na
kupokelewa na Mh. Waziri mkuu Mizengo Pinda (hayupo
pichani).
Meza Kuu ikipokea
maandamano ya Wanafunzi na Taasisi mbalimbali za Kiserikali na zisizo za
Kiserikali wakati sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu
zilizofanyika jijini Dar leo.
Jaji Kiongozi (Mstaafu)
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh.Amiri Ramadhani
Manento akisoma hotuba yake katika maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu
ambapo aliwasilisha Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa nchi zote
zihakikishe kuwa zinafuata maazimio ya tamko la haki za binadamu na wananchi
wake wanufaike na haki zilizomo ndani yake.
Mwanasheria Mkuu wa
Sreikali Jaji Frederick Werema akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Haki za
Binadamu.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akizungumza
kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa ambapo amesema chini ya mpango
wa pamoja, Umoja wa Mataifa nchini Tanzania unasaidia vitengo muhimu vya
serikali na wadau wengine wa mzunguko wa Haki za Binadamu, kwa mfano ofisi ya
Mwanasheria Mkuu, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na idadi kubwa ya
Asasi zisizo za kiserikali zinazohusika na masuala ya Haki za
Binadamu.
Vilevile amesema Umoja wa
Mataifa unaendelea kuinga mkono serikali kufuatilia ahadi zilizotolewa kwa
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na mapendekezo yakiwemo kutoka
katika Bodi za Mikataba ya haki za Binadamu.
Afisa Mipango kutoka Ofisi
ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Kanda ya Afrika Mashariki Bw. Abdu
Mohammed akisoma hotuba kwa niaba ya Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa
Mataifa ambapo amesisitiza kila raia anapaswa kuwa na haki na fursa ya kushiriki
katika masuala ya umma, moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi huru wa
kuchaguliwa, pia kila binadamu ana haki ya kupiga kura na kuchaguli na na kuweza
kufikia huduma za kijamii sambamba uhuru wa kujieleza, kukusanyika na
kuungana.
Amongeza kuwa haki hizi
zinatakiwa kumhusu kila mtu na hakuna hata mmoja atakaye baguliwa kwa moja kati
ya hizo kwa sababu ni mwanamke, au anatoka katika kundi dogo, au anaabudu katika
dini Fulani, au kwa sababu ni shoga, au ana ulemavu, anaamini siasa Fulani, au
mkimbizi au ana rangi fulani, anatoka katika kabila
Fulani.
Mgeni rasmi Mh. Waziri Mkuu
Mizengo Pinda akisoma hotuba yake ambapo amesema Pamoja na kuadhimisha
kumbukumbu ya Siku ya Haki za Binadamu, pia tunaadhimisha kumbukumbu ya Siku ya
Kimataifa ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa pamoja. Kaulimbiu ya mwaka huu
katika Kupambana na Rushwa ni “Unaweza kuzuia rushwa, chukua hatua sasa”. Kauli
hii inaonesha umuhimu wa Wananchi wa rika zote kupiga vita
rushwa.
Mh. Pinda amesema hatua ya
kuunganisha maadhimisho haya na kufanyika sehemu moja kunapunguza gharama kwa
upande wa Serikali, na pia kunatoa nafasi kwa Wananchi kufahamu umuhimu wa siku
zote mbili bila kulazimika kuondoka eneo moja la tukio kwenda eneo jingine.
Napenda kuzipongeza Taasisi zote husika kwa kuunganisha matukio haya mawili na
kuadhimisha sehemu moja na kwa wakati mmoja.
Ameongeza kuwa Huu ni mwaka
wa tano tangu Taifa letu lilipoanza kuadhimisha siku hii Kitaifa. Kaulimbiu ya
Kimataifa kwa mwaka huu ni: “Sauti yangu inachangia” (My voice counts). Ujumbe
huu unatukumbusha kushiriki katika kutoa maoni katika shughuli mbalimbali za
Kijamii au Kitaifa.
Mh. Waziri mkuu Mizengo
Pinda akizindua taarifa ya miaka 10 ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
(THBUB). Wanaoshuhudia uzinduzi huo ni Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Mathias
Chikawe (kushoto) na Naibu wake Mh. Angellah Kairuki
(kulia).
Sasa imezinduliwa
rasmi….Mh. Waziri mkuu Pinda akionyesha ripoti hiyo kwa wageni waalikwa (hawapo
pichani). Kulia ni Jaji Kiongozi (Mstaafu) Mwenyekiti wa Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora Mh.Amiri Ramadhani Manento na Kushoto ni Waziri wa
Katiba na Sheria Mh. Mathias Chikawe (kushoto).
Waziri Mkuu Pinda akipitia
ripoti hiyo.
Mkurugenzi Mkazi
wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot
akipitia nakala taarifa ya miaka 10 ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora.
Kikundi cha Wana wandime ya
kwetu ngoma wakitoa burudani wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za
Binadamu yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
leo.
Pichani Juu na Chini ni
Wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za serikali, Wanafunzi
wa shule za Sekondari, Wadau wa Haki za Binadamu na Wananchi wakati wa sherehe
za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu.
Mgeni rasmi Waziri Mkuu
Mizengo Pinda katika picha ya pamoja na Viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na
Waziri wa Katiba na Sheria na Naibu wake.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda
akiagana na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh.
Mahfoudha Alley Hamid.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda
akiondoka katika viwanja vya Mnazi Mmoja baada ya sherehe za maadhimisho ya Siku
ya Haki za Binadamu huku akisindikizwa na Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Naibu Waziri
wa Katiba na Sheria na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali.
Post a Comment