Ahoji Dk. Slaa
kairudisha lini na wapi?
*Awaita waganga njaa si wanasiasa
*Awaita waganga njaa si wanasiasa
MWANZA,TANZANIA
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi
na Uenez Nape Nnauye, amerusha kombora kuwa vigogo wengi ndani ya CHADEMA
wameendelea kuwa na kadi za CCM na wengine wanaendelea kuzilipia, jambo
linalothibitisha unafiki walionao viongozi wengi wa upinzani
nchini.
Akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM
wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza, leo uliokuwa na lengo la kupokea maazimio ya
Mkutano Mkuu wa nane wa CCM na hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya
Kikwete, Nape amedai siasa kwa sasa imevamiwa na makanjanja wengi ambao kazi yao
ni kuganga njaa na hivyo huishi kinafiki kwakuwa wakisemacho sicho
wanachokiishi.
Sambamba na kombora hilo, Nape ameitaka CCM
kuhakikisha inatoa uongozi mzuri ili kudhibiti uvamizi huu wa makanjanja kwenye
siasa za hapa nchini.
"Siasa leo imevamiwa na makanjanja waganga njaa,
ambao kwakweli wanachosema na wanachotenda ni vitu viwili tofauti, hawaishi
maneno yao. Tunao viongozi wengi wa Chadema ambao kucha kutwa wanaishambulia CCM
kwa maneno wakati tunawaona wakija kulipia kadi zao za CCM" alisema
Nape.
"Kama nasema uongo, Babu Dk. Slaa ajitokeze
aseme kadi yake ya CCM aliirudisha lini na kumkabidhi nani. Lakini ninayo orodha
ya vigogo kibao wa Chadema ambao huja kulipia kadi zao za CCM kila mara. Huu ni
unafiki mkubwa" alisisitiza Nape.
Nape alisema kauli ya Dk. Slaa kudai kwamba
anataka kukisafisha Chadema kwa madai kuwa kuna viongozi wa chama hicho ngazi za
chini ambao ni mamluki waliopandikizwa na CCM, ni kuweweseka vibaya kwa kuwa
wenye kadi za CCM si viongozi hao wadogo tu, hata vigogo wa juu kabisa wa
Chadema wana kadi za CCM, hivyo awe makini asije kujikuta anajifukuza na yeye
kwa kuwa hakumbuki ni lini alirudisha kadi ya CCM.
Kuhusu DK. Slaa kuitupia tuhuma mbalimbali
sekretarite mpya ya CCM, Nape anasema anamshangaa kushughulika na uongozi ndani
ya CCM badala ya kujenga Chama chake ambako kinamsambarakitikia mikononi kila
kukicha.
"Sana huyu Babu, hivi yeye badala ya kujenga
chama chake ambacho kinamsambaratikia mikononi kila siku anaweweseka na
sekretariete mpya ya CCM, nani kampa kazi ya kuitathimini sekretariti mpya ya
CCM?" alishangaa Nape.
Nape aliwapongeza viongozi wa CCM wilaya ya
Nyamagana kwa aina ya mkutano wa Halmashauri Kuu ya wilaya waliyoitisha katika
mkakati wa kuendeleza yale yaliyoamuliwa na mkutano mkuu wa CCM
taifa.
"Palianza kujengeka utamaduni wa baada ya
kufanya maamuzi kwenye vikao hakuna utaratibu wa ngazi za chini kuyachukua
maamuzi na kuweka mkakati wa kuyatekeleza, nyie Nyamagana mmefungua ukurasa
mpya, nawapongeza na kuagiza wilaya zote nchini na ngazi zingine za chama kuiga
mfano huu mzuri wa Nyamagana" alisema Nape.
Aidha amesisitiza agizo la Katibu Mkuu wa CCM
Abdulrahman Kinana kuwa ni lazima kuitoa CCM ofisini na kuipeleka kwa watu kama
njia ya kuwa karibu zaidi na watu na kujua matatizo yao na kisha kuyatafutia
ufumbuzi.
"Nasisitiza viongozi wa ofisini hatuwataki kwa
sasa, lazima kutekeleza kwa vitendo agizo la katibu mkuu la kutoka ofisini na
kuipeleka CCM kwa watu, mtaani kuwasikiliza, kujua matatizo yao na kuyatafutia
ufumbuzi." alisema Nape.
Post a Comment