Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila
maarufu kama RAY C akimshukuru Rais Kikwete kwa kumsaidia
matibabu,alipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na
Ray C watu kushoto,Mama yake mzazi Ray C Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na
kulia ni Sarah Mtweve Dada yake Ray C.Picha na Freddy
Maro
*********
*********
Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila
maarufu kama RAY C leo amemtembelea Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini
Dare s Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu wakati alipokuwa mgonjwa hivi
karibuni.
Rehema aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth
Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na
kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake.Kwa
apande wake ,Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya
mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwaajili ya
mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa na
Rais.
Post a Comment