Redds Miss
Tanzania 2012 Brigitte Alfred ameondoka jijini Dar es Salaam, leo tarehe 12
Desemba 2012 kuelekea mkoani Kagera kwa shughuli za Jamii.
Mrembo
huyo wa Redds Miss Tanzania, akiwa mkoani Kagera atatembelea Shule maalum ya
Mugeza Mseto, inayofundisha wanafunzi wenye ulemavu, pia atatembelea Kituo cha
Nusura ambacho kinatunza watoto yatima.
Mrembo
Brigitte Alfred, ambaye pia ni Balozi wa Walemavu wa ngozi, [Albinos] atatoa
misaada ya kijamii katika vituo hivyo. Vifaa hivyo ni pamoja na Fimbo maalum za
kutembelea walemavu wasioona, Miwani, Kofia na Madawa ya ngozi kwa
ajili ya Walemavu wa ngozi. Pamoja na vyakula.
Redds
Miss Tanzania 2012 pia atatembelea Wilaya ya Misenyi na kutoa misaada kama hiyo
katika kituo kimoja kilichopo wilayani humo.
Ziara
ya Miss Tanzania 2012 imedhaminiwa na Optima Lodge & Safaris pamoja na
Victoria Perch Hotel zote za Mkoani Kagera.
Kabla ya
kurejea jijini DSM Redds Miss Tanzania 2012 ataelekea Mwanza kwa shughuli
zingine za kijamii.
Imetolewa
na:
HIDAN
.O. RICCO.
PRO.
0715 019288
Post a Comment