Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TAZAMA VIATU VIPYA ALIVYOBUNIWA LIONEL MESSI NA SHABIKI WAKE ILI ATUPIE KATIKA MECHI YA LA LIGA KESHO J'PILI DHIDI YA ATLETICO MADRID YA KINA FALCAO...!

 


Viatu vilivyobuniwa na shabiki na kuvaliwa na Messi kesho katika mechi ya Barcelona dhidi ya Atletico Madrid katika La Liga, Ligi Kuu ya Hispania.
Kwa viatu hivi Gerd Muller nitamuacha sana kwa rekodi ya mabo...! Messi akiangalia mitindo ya viatu kabla ya kuchagua atakavyovaa kesho Desemba 16, 2012 dhidi ya Atletico Madrid.
Viatu vilivyobuniwa na shabiki na kuvaliwa na Messi kesho katika mechi ya Barcelona dhidi ya Atletico Madrid katika La Liga, Ligi Kuu ya Hispania.
BARCELONA, Hispania
Wakati Lionel Messi wa Barcelona akiingia dimbani na tmu yake kesho usiku (Jumapili Desema 16, 2012) kucheza mechi ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania dhidi ya Atletico Madrid ya kina Radamel Falcao, atakuwa amevaa viatu vilivyobuniwa na shabiki wake, imefahamika.



Shabiki huyo aitwaye Javier Pascual Mullor ndiye aliyebuni muonekano wa viatu vya "adidas adizero f50s" vitakavyotangazwa duniani kesho, shukrani kwa uamuzi wa Messi wa kuvichagua kwa mechi ya kesho.

Zaidi ya watu 14,200 waliwasilisha mapendekezo yao baada ya ukurasa wa Messi wa mtandao wa kijamii wa facebook kuwataka watume mapendekezo yao.

Mtindo aliobuni Mullor una logo ya Messi , bendera ya Argentina, 'Leo 10' na 'Thiago', jina la mtoto wa kiume ambaye ni wa kwanza wa Messi aliyezaliwa hivi karibuni.

Messi alizungumzia viatu hivyo leo kwa kusema: 'Nimefurahi kuwa na viatu hivi vya "miadidas boots" nan ninapenda kumpongeza Javier kwa ubunifu wake na nitavivaa Jumapili (kesho) katika mechi yetu dhidi ya Atlético Madrid.

'Nachukua fursa hii pia kumshukuru kila mmoja aliyetuma ubunifu wake, wote wametuma mitindo mizuri!'

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top