Mwadishi Mashuhuri wa Makala mbalimbali na habari za
Kimahakama Happiness Katabazi(Kulia)akiwa na 'mkwe wake 'ACP-Abdallah Zombe leo
asubuhi katika Mahakama ya Rufaa Dar es Salaam, muda mfupi baada ya rufaa
iliyokatwa na DPP-Dk.Elezer Feleshi kupinga hukumu ya kesi ya mauaji ya watu
wanne dhidi ya Zombe na wenzake kushindwa kusikilizwa na mahakama hiyo kwasababu
jaji mmoja kati ya majaji watatu wanaosilikiza kesi hiyo anaumwa.
Wakili Mwandamizi wa
Serikali Angaza Mwipopo akisalimiana ACP-Abdallah Zombe leo asuhubi ndani ya
Mahakama ya Rufaa
Hii ndiyo timu ya mawakili
waandamizi wa serikali katika rufaa ya Zombe Timoth Vitalis, Edwin
Kakolaki,Angaza Mwipopo,Prudence Rweyongeza,Alexander Mzikilia,Mgaya Mtaki na
Peter Njike, wakiwa ndani ya ukumbi wa mahakama ya rufaa Dar es Salaam, lakini
hata hivyo rufaa hiyo haikuweza kusikilizwa kwasababu jaji mmoja anayeunda jopo
la majaji wa tatu anaumwa.
Zombe na wakili wake
Richard Rweyongeza.Na upande wa jamhuri unawakilishwa na timu ya mawakili
waandamizi wa serikali saba.Picha na Happiness Katabazi
--
Na Happiness
Katabazi
MAHAKAMA ya Rufaa Dar es Salaam, jana ilishindwa kuanza kusikiliza rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP), Dk.Eliezer Feleshi dhidi ya aliyekuwa M kuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi(ACP),Abdallah Zombe na wenzake kwasababu jaji mmoja ambaye anaunda jopo la majaji wa tatu Semistocles Kaijage anaumwa.
DPP.Feleshi anapinga hukumu
iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Jaji Salum Massati ambaye
kwasasa ni jaji wa mahakama ya rufaa kwasababu hukumu ile ina makosa ya kisheria
na kwamba jaji Masati akupaswa kuwaachilia huru wajibu rufaa hao na Jaji Natalia
Kimaro ndiyo aliarisha rufaa hiyo leo asubuhi na kuzieleza pande zote mbili kuwa
tarehe ya kuja kusikilizwa rufaa hiyo watapatiwa kwa maandishi.
Post a Comment