MWENYEKITI wa WAMA Mama
Salma Kikwete wito kwa wananchi tabia ya kujisomea vitambu na machapisho
mbalimbali ili kujiongezea maarifa yatakayowawezesha kujiletea
maendeleo.
Mama Kikwete alitoa
kauli hiyo kwenye Makumbusho ya Taifa leo jijini Dar es salaam wakati wa
uzinduzi wa makatba kwa ajili ya watoto na watu wazima.
Alisema kuwa elimu ndio
silaha pekee ya kukabiliana na maadui watu ambao ni ujinga,maradhi na umaskini
na hivyo kujiletea maendeleo.
Mama Kikwete aliongezea
mbinu za kujiendeleza kimaisha zinapatikana pia kwa njia elimu kupitia vitabu
na machapisho mbalimbali yanayopatikana kwenye maktaba mbalimbali ndani na nje
ya Tanzania.
Alisema kuwa hiyo
itasaidia katika kuongeza maarifa kwani kutakuwa na vitabu,kompyuta na mitambo
ya mawasiliano ambayo itawawezesha watumiaji kupata elimu ya taaluma
mbalimbali.
Aidha Mama Kikwete
aliwasihi watumishi wa Makumbusho hiyo kuwa ni jukumu lao kutunza maktaba hiyo
ili isaidie kukidhi malengo ya kuanzishwa kwake kwa kuandaa taratibu bora za
kudhibiti matumizi yasiyo na tija ya maktaba ikiwemo upotevu machapisho na
vitabu mbalimbali na uhalibifu wa vitabu unaofanywa na watu wasiotaka
maendeleo.
Mwenyekiti huyo WAMA
alimshukru Balozi wa Korea Kusini Young Shimo Dho kwa niaba ya nchi yake kwa
msaada wa vitabu na vifaa mbalimbali kwa ajili ya maktaba hizo mbili
.


Post a Comment