Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akimfariji mmoja kati ya abiria waliokua katika
Jahazi la Sun Rise, Juma Ali Jaku , iliyopata ajali na
kuzama kati ya Tanga na Mkokotoni
karibu na Mkondo wa Nungwi, ikiwa imebeba jumla ya abiria 32 kati ya hao 21
wameokolewa na 11 kati yao hadi sasa hawajapatikana. Kushoto kwa Balozi Seif ni
Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mh. Pemba Juma
Khamis.
Nahodha wa Jahazi ya Sun
Rise, iliyozama kati ya Tanga na
Mkokotoni, karibu na Mkondo a Nungwi, Abdulla Saleh, akimuelezea Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, jinsi mkasa huo ulivyowatokea na
kuzama baada ya chombo chao kupatwa na dhoruba kali.
**************************************
Nahodha
na abiria mmoja ambao ni miongoni mwa watu 21 walionusurika
kufa kati ya 32 waliokuwa wakisafiri na Jahazi lililopata ajali na kuzama
liitwalo Sun Rise likitokea Mkoani Tanga kuja Mkokotoni Unguja, wakiwa katika
wodi ya Hospitali ya Wilaya
ya Kaskazini A iliyopo Kivunge,
Zanzibar wakiendelea kupatiwa matibabu.
Jumla ya
abiria 21 wameokolewa katika ajali hiyo na kupelekwa Kivunge kwa ajili ya
kupatiwa huduma ya matibabu ambapo hadi sasa abiria saba watoto wakiwa watatu na
watu wazima wane bado hawajapatikana
kutokana na ajali hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na Viongozi wa Juu wa Ofisi yake
ambayo ndio inayoratibu masuala ya maafa walifika Hospitali ya Kivunge kuwapa
pole majeruhi hao waliobakiwa wakipatiwa huduma za
Matibabu.
Nahodha
wa Jahazi hiyo Bwana Abdulla Saleh akiwa pamoja na Majeruhi mwenzake Bwana Ali
Juma Jaku alimueleza Balozi Seif kwamba ajali hiyo ilitokea kutokana na
kuchafuka mara Moja hali ya Bahari.
Nahodha
Abdulla alisema chombo chao chenye uwezo wa kubeba abiria 50 kiliondoka
bandarini Tanga salama Majira ya Saa nane za Usiku na walianza kupata
mitihani na kuzama mara baada ya kuchafuka kwa bahari majira ya saa 11 za
alfajiri.
Akiwapa
pole majeruhi hao Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar Balozi Seif alisema juhudi alizoonyesha
Nahodha huyo katika kusaidia uokozi huo zinastahiki kupongeza na Jamii
yote.
Balozi Seif aliwaombea
majeruhi hao kupoa haraka na kuungana na familia zao na kuutaka Uongozi wa
Hospitali ya Kivunge kuendelea kuwachunguza Mareruhi hao kutokana na juhudi
kubwa waliyoifanya ya kusaidia harakati za uokozi wa wenzao uliopelekea kupoteza
nguvu nyingi.
Jahazi
hilo la Sun Rise lililokuwa likitokea Tanga kuja Mkokotoni mbali ya kuchukuwa
abiria pia lilibeba sanduku nne za maziwa pamoja na Polo zipatazo 30 za
Mkaa.
Othmna Khamis
Ame
Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
31/1/2013.
Post a Comment