Bunge la Marekani limeupitisha mswada wa kuiepusha Marekani kuingia katika mdodoro wa uchumi
Mswada huo uliotayarishwa na Seneti unatarajiwa kutiwa saini haraka na Rais Obama na kuwa sheria.
Kulingana na mswada huo wa mwafaka, kodi zitapandishwa kwa Wamarekani wenye mapato yanayovuka dola laki nne na nusu kwa mwaka. Mswada huo pia unairuhusu serikali kuendelea na matumizi.
Hata hiyvo wajumbe wa chama cha Republican walitafakari wazo la kuongeza katika mswada huo, kipengele juu ya kukata matumizi. Lakini wajumbe hao hawakuweza kupata uungaji mkono wa kutosha.