Umoja wa Mataifa na washirika wake wameomba dola za kimarekani milioni 30.5 kuwasaidia zaidi ya watu laki 5 walioathiriwa na vita mkoani Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Nesirky amesema mpango huo ulioanzishwa leo mjini Goma unalenga kufadhili shughuli za kibinadamu za kuokoa maisha katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu.
Alisema mpango huo ni pamoja na juhudi za kuhakikisha watu wanaoishi kwenye kambi baada ya kupoteza makazi yao wanapata chakula , maji na makazi pamoja na kusaidia familia kurudi makwao na kujenga upya maisha yao. Washirika wa mambo ya afya wanapanga kuzifanyia ukarabati kliniki na vituo vya afya na pia kuleta dawa zaidi.
Post a Comment