Katika hali isiyokuwa ya
kawaida kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa soko kuu la jijini Mwanza leo amezuwa
sokomoko na taharuki kwa wafanyabiashara wa soko hilo mara baada ya kukutwa na
jeneza la kusafirishia maiti katika sehemu yake ya biashara tena juu ya magunia
ya viazi sokoni hapo.
Aliyezua taharuki hilo
ni mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko kuu la jijini Mwanza ambaye pia ni
mfanyabiashara wa viazi wa soko hilo Bw. Hamad Nchola ambaye alikuwa hakuwa na
majibu ya moja kwa moja balimajibu mafupi mafupi yasiyoridhisha wakati akihojiwa
na waandishi wa habari.
Baadhi ya
wafanyabiashara na wanunuzi wakijadiliana juu ya kuwepo kwa jeneza hilo katika
eneo la banda la biashara la mwenyekiti soko kuu la
Mwanza.
Jeneza
juu ya magunia ya viazi ndani ya banda la biashara la
mwenyekiti.
Bw.
Hamad Nchola ambaye ni mwenyekiti wa wafanyabiashara soko
kuu la Mwanza aliyezua
balaa.
Naye Mwenyekiti huyo
akijitetea kuhusu sakata hilo amesema kuwa aliamua kufanya uamuzi huo wa
kuhifadhi jeneza hilo sokoni hapo kwenye sehemu yake ya biashara mara baada ya
kulichukuwa kutoka msikitini akisubiri usafiri kulipeleka hospitali ya Rufaa ya
Bugando kuuchukuwa mwili wa mke wa mfanyabiashara mwenzake sokoni hapo ambao
ulipaswa kusafirishwa kuelekea wilayani Magu kwa
mazishi.
Alipohojiwa kwa nini
asingeliacha jeneza hilo msikitini au kulipeleka nyumbani kusubiri muda muafaka
badala ya kulihifadhi sokoni hapo ambako kunatambulika kuwa ni sehemu mahususi
kwaajili ya biashara ya mazao na chakula pamoja na kuwa na watu wenye imani
tofauti, mfanyabiashara huyo alisema aliamua kufanya hivyo kwakuwa hakuona shida
na alifanya hivyo kama wafanyabiasha wengine na kwamba inshu hiyo imekuwa kubwa
kwa kuwa yeye ni kiongozi.
Kisha akaongeza kuwa
kufanya hivyo siyo tatizo na jeneza hilo ni mbao tu na siyo kitu cha
kustaajabisha na aliamua kulihifadhi eneo la biashara yake kwa kuhofia kuwa
lingenyeshewa na mvua.
Baadhi
ya wafanyabiashara na wanunuzi wakichungulia eneo la banda la biashara la
mwenyekiti ambapo kuna jeneza
hilo.
Pamoja na kuwa na
kigugumizi kujibu kuhusu muda alilolileta jeneza hilo sokoni hapo kwamujibu wa
mmoja wa walinzi ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa jeneza hilo
liliingia sokoni hapo mapema alfajiri wakati hakukuwa na wafanyabiashara sokoni
hapo hali ambayo ilimshitua na mlinzi huyo akashindwa kuhoji kwakuwa ni
mfanyabisha huyo ni bosi wake.
Hata hivyo baadhi ya
wafanyabiashara waislamu wamepinga vikali kuwa jeneza hilo si mali ya misikiti
kwa kuwa waumini hao hawatumii masanduku ya miundo hiyo hususani hilo lenye
tundu la kuagia, zaidi ya kutumia majeneza yenye mikono minne hivyo wamemtaka
kiongozi huyo kuhojiwa zaidi juu ya sakata
hilo.
Vijana
wakifanya mchakato kuliondoa jeneza hilosokoni hapo toka kwenye banda la
biashara la mwenyekiti.
Hatimaye Jeneza hilo
liliondoshwa sokoni hapo na vijana waliolibeba msobemsobe kwenye majira ya saa 4
asubuhi ya leo lisijulikane lilipoelekea.
Mwendo
msobemsobe.
Katika hali isiyokuwa ya
kawaida kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa soko kuu la jijini Mwanza leo amezuwa
sokomoko na taharuki kwa wafanyabiashara wa soko hilo mara baada ya kukutwa na
jeneza la kusafirishia maiti katika sehemu yake ya biashara tena juu ya magunia
ya viazi sokoni hapo.
Aliyezua taharuki hilo
ni mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko kuu la jijini Mwanza ambaye pia ni
mfanyabiashara wa viazi wa soko hilo Bw. Hamad Nchola ambaye alikuwa hakuwa na
majibu ya moja kwa moja balimajibu mafupi mafupi yasiyoridhisha wakati akihojiwa
na waandishi wa habari.
Baadhi ya wafanyabiashara na wanunuzi wakijadiliana juu ya kuwepo kwa jeneza hilo katika eneo la banda la biashara la mwenyekiti soko kuu la Mwanza. |
Jeneza juu ya magunia ya viazi ndani ya banda la biashara la mwenyekiti. |
Bw. Hamad Nchola ambaye ni mwenyekiti wa wafanyabiashara soko kuu la Mwanza aliyezua balaa. |
Naye Mwenyekiti huyo
akijitetea kuhusu sakata hilo amesema kuwa aliamua kufanya uamuzi huo wa
kuhifadhi jeneza hilo sokoni hapo kwenye sehemu yake ya biashara mara baada ya
kulichukuwa kutoka msikitini akisubiri usafiri kulipeleka hospitali ya Rufaa ya
Bugando kuuchukuwa mwili wa mke wa mfanyabiashara mwenzake sokoni hapo ambao
ulipaswa kusafirishwa kuelekea wilayani Magu kwa
mazishi.
Alipohojiwa kwa nini
asingeliacha jeneza hilo msikitini au kulipeleka nyumbani kusubiri muda muafaka
badala ya kulihifadhi sokoni hapo ambako kunatambulika kuwa ni sehemu mahususi
kwaajili ya biashara ya mazao na chakula pamoja na kuwa na watu wenye imani
tofauti, mfanyabiashara huyo alisema aliamua kufanya hivyo kwakuwa hakuona shida
na alifanya hivyo kama wafanyabiasha wengine na kwamba inshu hiyo imekuwa kubwa
kwa kuwa yeye ni kiongozi.
Kisha akaongeza kuwa
kufanya hivyo siyo tatizo na jeneza hilo ni mbao tu na siyo kitu cha
kustaajabisha na aliamua kulihifadhi eneo la biashara yake kwa kuhofia kuwa
lingenyeshewa na mvua.
Baadhi ya wafanyabiashara na wanunuzi wakichungulia eneo la banda la biashara la mwenyekiti ambapo kuna jeneza hilo. |
Pamoja na kuwa na
kigugumizi kujibu kuhusu muda alilolileta jeneza hilo sokoni hapo kwamujibu wa
mmoja wa walinzi ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa jeneza hilo
liliingia sokoni hapo mapema alfajiri wakati hakukuwa na wafanyabiashara sokoni
hapo hali ambayo ilimshitua na mlinzi huyo akashindwa kuhoji kwakuwa ni
mfanyabisha huyo ni bosi wake.
Hata hivyo baadhi ya
wafanyabiashara waislamu wamepinga vikali kuwa jeneza hilo si mali ya misikiti
kwa kuwa waumini hao hawatumii masanduku ya miundo hiyo hususani hilo lenye
tundu la kuagia, zaidi ya kutumia majeneza yenye mikono minne hivyo wamemtaka
kiongozi huyo kuhojiwa zaidi juu ya sakata
hilo.
Vijana wakifanya mchakato kuliondoa jeneza hilosokoni hapo toka kwenye banda la biashara la mwenyekiti. |
Hatimaye Jeneza hilo
liliondoshwa sokoni hapo na vijana waliolibeba msobemsobe kwenye majira ya saa 4
asubuhi ya leo lisijulikane lilipoelekea.
Mwendo msobemsobe. |
Post a Comment