Mkurugenzi Mkuu wa Tehama akifungua semina ya Mkongo
wa Mawasiliano iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam na kuwashirikisha wahariri
wa vyombo mbalimba vya habari. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni
simu Tanzania (TTCL), Said Amir Said na Meneja Uendeshaji wa kampuni hiyo, Adin
Mgendi. (Picha na John Dande wa Habari Mseto Blog)
Kulia ni
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni simu Tanzania (TTCL), Said Amir Said.
akifafanua jambo wakati wa semina
ya Mkongo wa Mawasiliano iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam na kuwashirikisha
wahariri wa vyombo mbalimba vya habari. Kushoto
ni Meneja Uendeshaji wa kampuni hiyo, Adin Mgendi.
Baadhi ya Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya
habari wakiwa katika semina hiyo.
DAR ES SALAAM,
Tanzania
SERIKALI imesema kuwa mradi
wa mkongo wa Taifa wa mawasiliano ukisimamiwa na kuendeshwa kwa uaminifu
utachangia maendeleo ya nchi ikiwemo kulipa mkopo uliotumika
kuujenga.
Mradi huo ambao utapanua soko
la mawasiliano kutoka nchi moja hadi tisa.
Akizungumza ijini Dar es
Salaam leo wakati wa kufungua semina ya wahariri wa vyombo vya habari Mkurugenzi
wa Tehama, Injinia Zaipuna Yonah, alisema kuwa manufaa ya mkongo huo wa
mawasiliano yameshaanza kuonekana hasa baada ya kuongezeka ubora na kasi ya
matumizi ya mtandao na data pamoja na utoaji wa huduma za elimu
mtandao.
Yonah alisema kuwa faida za
mkongo zinaonekana na zimekidhi matarajio ya Serikali ya kuziba pengo la
matumizi ya Tehama kwa wananchi na kukuza uchumi.
Akizitaja changamoto
zilizojitokeza alisema kuwa ni usalama wa miundo mbinu ambayo inapita kwenye
makazi ya watu, mashambani, hifadhi za wanyama na kuwataka watanzania
kuhakikisha rasilimali niyo inatunzwa.
Pia alisema kuwa Serikali
imeikabidhi kampuni ya simu (TTCL) kuhakikisha inasimamia, inaendesha na
kuuendeleza mkongo wa mawasiliano ili kuleta mabadiliko ya utendaji na ufanisi
wa kazi kupitia Serikali mtandao, elimu mtandao, afya mtandao, kilimo mtandao na
kujenga utamaduni mpya wa wanachi kupata taarifaza serikali kwa
uwazi.
Post a Comment