HIFADHI
ZA TAIFA TANZANIA
PRESS
RELEASE
AJALI YA RADI YAUA MTALII MMOJA MLIMA
KILIMANJARO
Mgeni mmoja raia wa
Ireland anayefahamika kama Ian Mc Keever amefariki dunia jana tarehe 2.1.2013
majira ya saa sita na nusu mchana baada ya kutokea kwa ajali ya
radi kali wakati akipanda Mlima Kilimanjaro akiwa pamoja na
wenzake.
Ajali hiyo ya radi
ilitokea katika eneo la Kibao cha Moir Hut katika njia ya Londorosi. Aidha,
wageni wengine wanne walijeruhiwa katika ajali
hiyo.
Marehemu Mc Keever
mwenye umri wa miaka 42 alifika nchini kwa ajili ya shughuli ya utalii ya
kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia Kampuni ya Wakala wa Utalii ya Everlasting
Tour Company Limited ya Mjini Arusha ambapo marehemu pamoja na wenzake walianza
safari yao ya kupanda mlima tarehe
30.12.2012
Baada ya kutokea kwa
ajali hiyo wageni wengine 21 waliokuwa pamoja waliamua kuahirisha safari yao ya
kupanda mlima.
Shirika la Hifadhi za
Taifa (TANAPA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Wakala wa Utalii ya Everlasting
zinaendelea na taratibu mbalimbali za kushughulikia ajali hii pamoja na matibabu
kwa waliojeruhiwa.
Imetolewa
na
Pascal
Shelutete
Meneja
Uhusiano
HIFADHI ZA TAIFA
TANZANIA
03.01.2013
Post a Comment