
Mkutano
huo ambao ni wa kwanza kwa uongozi wa Manji uliochaguliwa Julai 15,
mwaka jana, utajadili mambo mbalimbali ya maendeleo ya klabu hiyo kongwe
nchini.
Awali,
mkutano huo ulikuwa ufanyike Desemba 8, mwaka jana, lakini ukasogezwa
kupisha sherehe za miaka 51 ya uhuru ambapo kilele chake kilifanyika
Desemba 9.
Kwa
mujibu wa Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Lawrance Mwalusako, maandalizi kwa
ajili ya mkutano huo utakaoanza saa mbili asubuhi yamekamilika ambapo
amewaomba wanachama kujitokeza kwa wingi kujadili mipango mbalimbali ya
maendeleo.
“Huo
ni mkutano wa wanachama hivyo kutajadiliwa masuala mengi ambayo
yatajitokeza hukohuko kwenye mkutano, tunawaomba wana-Yanga kujitokeza
kwa wingi,” alisema.
Post a Comment