Afisa uhusiano na matukio
wa Airtel Tanzania Dangio Kaniki akimvalisha sare za shule na viatu mwananfunzi
wa shule ya msingi Kiromo zilizotolewa na Kampuni ya simu ya Airtel mwishoni mwa
wiki hii.Airtel metoa msaada wa sare za shule zikiwemo Kaptura 600 , skirt 600 ,
mashati 1193 na viatu 728 vyote vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 kwa shule
ya msingi Kiromo.
Meneja wa uhusiano wa
Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kushoto) akimkabidhi sare za shule Mwalimu mkuu
wa shule ya msingi Kiromo Nasib Pangahela mwishoni mwa wiki hii, akishuhudiwa
na meneja wa huduma kwa jamii (katikati) bi Hawa Bayumi.
Meneja wa uhusiano wa
Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kushoto) akimkabidhi mmoja wa wanafunzi wa
shule ya msingi Kiromo sare za shule zilizotolewa na Kampuni ya simu ya Airtel
mwishoni mwa wiki hii, akishuhudia makabidhiano hayo (wa pili kushoto) meneja wa
huduma kwa jamii bi Hawa Bayumi akifuatiwa na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi
Kiromo Nasib Pangahela, Airtel metoa msaada wa sare za shule zikiwemo Kaptura
600 , skirt 600 , mashati 1193 na viatu 728 vyote vyenye dhamani ya shilingi
milioni 50 kwa shule ya msingi Kiromo.
Afisa uhusiano na matukio
wa Airtel Tanzania Dangio Kaniki (Kulia) akimpongeza Mwalimu mkuu wa shule ya
msingi ya Kiromo (kulia) baada ya makabidhiano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki
hii wakishuhudiwa na meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel Hawa Bayumi (wa pili
kulia) akifuatiwa na mmoja wa wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo bi Zuwena
Salumu, Airtel metoa msaada wa sare za shule zikiwemo Kaptura 600 , skirt 600 ,
mashati 1193 na viatu 728 vyote vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 kwa shule
ya msingi Kiromo.
Airtel Tanzania yatembelea
shule ya Kiromo mwishoni mwa wiki hii na kukabidhi sare za shule pamoja na viatu
vyenye dhamani ya shilling milioni 50. Katika msaada huo Airtel imetoa sare za
shule zikiwemo Kaptura 600 , skirt 600 , mashati 1193 na viatu 728, hafla ya
makabidhiano ilifanyika katika shule hiyo iliyopo Kiromo
-Bagamoyo.
*** ***
Alhamisi 10 February 2013,
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa gharama nafuu zaidi Tanzania, leo
imegawa sare za shule pamoja viatu katika shule ya msingi Kiromo iliyopo
Bagamoyo ikiwa ni sehumu ya shughuli zao za kusaidia jamii.
Shule ya kiromo ni moja kati ya shule zilizofaidika na mpango wa shule yetu na kuingia kwenye ukarabati wa majengo na madarasa na kubadili mazingira ya shule na kutoa vifaa vya kufundishia pamoja na computer. sasa Airtel imetoa Sare na viatu vya shule kwa wanafunzi wote shuleni hapo.
Katika kauli iliyotoleawa na kampuni ya Airtel Tanzania kupitia Meneja shughuli za kijamii bi. Hawa Bayumi alisema” Airtel imedhamiria kuendelea kuisadia shule mbalimbali kwa kutoa vifaa mbalimbali ikiwepo vya kufundishia ili kuhakikisha elimu bora inatolewa kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla. Na leo tunaendelea kuboresha shule yetu ya Kiromo kwa kutoa msaada wa uniform na viatu kwa wanafunzi.
M msaada wa sare zashule
tunazoto ni pamoja na Kaptura 600 , skirt 600 , mashati 1193 na viatu 728 vyenye
dhamani ya shilingi milioni 50 kwa shule ya msingi Kiromo.
Airtel Tunayo malengo ya dhati kabisa katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu hapa nchini na kuhakikisha kiwango cha ufaulu kinaongezeka na upatikanaji wa vitabu kwa wanafunzi wa shule za sekondari.
Leo tunathibitisha dhamira
yetu ya kusaidia mashule kwa kutoa sare za shule na viatu Kiromo shule ya
msingi”, alisema Bayumi Airtel itaendelea kusaidia mashule kwa kutoa vitabu na
vifaa mbali mbali vya kufundishia ikiwa ni sehemu ya shughuli zetu za kusaidia
jamii, nia yetu ni kuwafikia shule nyingi zaidi katika mikoa yote ya Tanzania
aliongeza.
Kampuni ya simu ya Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia sekta ya elimu hapa nchini. Tangu tulipoanza mradi wa “ shule yetu” mpango wa kusaidia vitabu na vifaa vya shule , shule mbalimbali nchini zimeshafaidika na mradi huu mpaka sasa.
Post a Comment