Mamia ya waombolezaji
katika mji wa Bredasdorp, jimbo la Western Cape, Afrika Kusini, wamehudhuria
mazishi ya msichana aliyebakwa na gengi.
Wanaume watatu wamekamatwa kwa kuhusika na ubakaji na mauaji ya msichana huyo na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani juma lijalo.
Shambulio hilo la kikatili limezusha hasira na maandamano kumtaka Rais Jacob Zuma achukue hatua kupambana na visa vingi vya ubakaji nchini Afrika Kusini.
Post a Comment