MWANAFUNZI wa darasa la sita Shule ya Msingi Kasumulu, Kata ya Ngana, wilayani Kyela, Kaselema Mpale (14) ameuawa kikatili kwa kuchinjwa na kitu chenye ncha kali, kisha kunyofolewa baadhi ya viungo vyake sehemu ya mwili.
Mama mzazi wa
mwanafunzi huyo, Lucia Kamnyonge alisema tukio hilo lilitokea Februari 8,
mwaka huu saa 1:30 usiku, alipotumwa na baba yake kwenda nyumba ya jirani
kuchukua mpunga ambao ungetumika kwa chakula usiku.
Kamnyonge
alisema mtoto wake hakupatikanika hadi alipokutwa siku ya pili yake, akiwa
amechinjwa na kunyofolewa baadhi ya sehemu zake za mwili ambazo ni pua, mdomo,
jicho, kuondolewa sehemu zake za siri na kuchunwa ngozi ya kichwa karibu na
utosi na mwili wake kutundikwa juu ya mti.
Aliendelea kuwa
baada ya hali hiyo taarifa ilipelekwa ofisi ya serikali ya kijiji, uliitishwa
mkutano wa wananchi wote na walitawanyika kuanza kumtafuta mtoto huyo bila ya
mafanikio.
Baadaye, baba yake alimkuta juu ya mti akiwa ametundikwa kichwa chini miguu juu na viungo vyake hivyo vikiwa vimenyofolewa.
Baadaye, baba yake alimkuta juu ya mti akiwa ametundikwa kichwa chini miguu juu na viungo vyake hivyo vikiwa vimenyofolewa.
Mwenyekiti wa
Kitongoji cha Ibungumbati lilipotokea tukio hilo, Adam Mkese alidai tukio hilo
limewashtua na kwamba, mkutano wa kijiji ulioitishwa kwa dharura wananchi
walimhusisha baba mzazi wa mtoto huyo na mauaji hayo.
Mkese alidai
watu wa kijiji hicho walimhusisha kutokana na mazingira tata ya kifo chenyewe na
maelezo ya kujichanganya aliyoyatoa.
Ofisa mtendaji
wa kijiji hicho, Naomi Charles alidai kuna dalili za mzazi huyo kuhusishwa na
mauaji hayo na kwamba, polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi.
Mwenyekiti wa
kijiji hicho, Baruti Mwakasala alidai kuwa hali katika kijiji hicho siyo nzuri
na kushukuru polisi kwa hatua za haraka walizochukua.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na
kukiri kumshikilia baba mzazi wa mtoto huyo kwa uchunguzi
zaidi.
mbeya
mbeya
Post a Comment