Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata taarifa kutoka kwa
Balozi wa China Nchini Tanzania Lu Yuquing wakati wa sherehe hiyo iliyofanyika
Dar es Salaam. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Dkt Fenella Mukangara, na Kaimu Mkuu wa Mkoa, Pia Mkuu wa Wilaya ya
Ilala, Raymond Mushi.
Ofisa
mauzo wa Ecobank Jakline Nyangoe (kushoto) akifafanulia jambo wageni waliofika
katika banda la maonyesho la benki hiyo wakati wa sherehe ya mwaka wa Kichina
iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam Februari 3
2013.
Wakazi wa Dar es Salaam na
wageni mbalimbali wakiangalia bidhaa za benki ya Ecobank katika banda la
maonyesho la benki hiyo wakati wa sherehe ya mwaka wa Kichina zilizofanyika
katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.
W
akazi wa
Dar es Salaam na wageni mbalimbali wakiangalia bidhaa za benki ya Ecobank katika
banda la maonyesho la benki hiyo wakati wa sherehe ya mwaka wa Kichina
zilizofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es
Salaam.
*********************************
Ecobank Tanzania ambayo ni
mojawapo ya benki katika kundi la Ecobank Africa iliyo katika nchi 33 Africa,
inazidi kukuza uwezo wa
wanabiashara Tanzania katika kushiriki biashara kati ya
Tanzania naChina kwa
kupunguza garama za uendeshaji biashara kati ya nchi hizi.
Wakishiriki katika
sherehe ya mwaka mpya ya China Jumapili
hii katika viwanja vya Mnazi Mmoja,Ecobank ilionyesha nia yake
ya kusaidia jamii ya
waendesha biashara kati ya Tanzania na China
zikiwepo huduma zinazorahisisha wafanyabiashara wa
Tanzania na wawekezaji
wa Kichinakushiriki katika
uagizaji na mauzo ya nje kati ya nchi
hizi.
"Sisi tunayo nia ya kutoa huduma za garama nafuu na
kurahisisha upatikanaji wa bidhaa hizi kuwezesha sekta hii inayokua kwa kasi
sana.
katika mwongo uliopita
kumekuwa na uwekezaji wa $ 868 bilioni wa
china ndani ya Tanzania, huduma zetu zinajaza pengo la kurahisisha biashara hii
"anasema Bw EnochOsei-Safo, Mkurugenzi
Mtendaji Ecobank Tanzania.
Ecobank inazindua huduma ya
kubadilisha hela ya Tanzania kupata sarafu za kichina (RMB) moja kwa moja,
ambapo hapo awali hapa Tanzania, wanabiashara walilazimika kubadili TZS kwa Dola
za kimarekani ili kununua RMB. Katika mfumo huo wa awali, wanabiashara
walipoteza kiasi kikubwa cha mtaji lakini sasa, Ecobank itatwawezesha
wanabiashara kupunguza garama hizi kwa kueneza huduma hii hapa
Tanzania.
" Sisi hatuwezi kupuuza matokeo ya biashara
ya China juu ya Afrika, ambayo
inafikia zaidi ya dolabilioni
200 katika mwaka 2012 kwa
uagizaji na 5% ya mauzo yote ya
Afrika kwenda nchini China, ushirikishwaji wa
kifedha kukuza sekta
hii ni muhimu, na ndiyo
maana Ecobank Groupimeonyesha
nia ya kurahisisha uendeshaji wa biashara
hii na kuwezesha Afrika kuwa na
ushindani na nchi zingine duniani.” Enoch
aliongeza.
Ecobank Tanzania katika miezi
michache ijayo itakua kituo cha kutoa huduma za uendeshaji biashara kati ya
Tanzania na China kwa kutoa huduma ya ubadilishaji wa sarafu ya kichina na pia
kulipia kodi ya forodhani kwa TRA papo kwa papo kupitia huduma ya Asybank katika
matawi yote ya Ecobank.
Kwa maelezo zaidi,
tembelea: www.ecobank.com
Post a Comment