Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

 


Baadhi ya Maafisa Habari Mawasiliano Serikalini wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge.
Baadhi ya Maafisa Habari Mawasiliano Serikalini wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene (kutoka kushoto wanne mstari wa mbele). Wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge leo kuangalia shughuli za Bunge Dodoma.
Baadhi ya Maafisa Habari Mawasiliano Serikalini wakielekea katika Ukumbi wa Mkutano wa Bunge leo Dodoma. Maafisa hao wamefanya ziara Bungeni hapo ili kuona shughuli za Bunge.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Aggrey Mwanri akiwakilisha hati mezani kuhusu Taarifa ya Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa na Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha,2010/2011.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Pereira Silima akiwasilisha azimio la Bunge la Kujiunga na Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia Vitendo vya Ugaidi wa Kutumia Nyuklia. Azimio hilo limeungwa mkono leo katika mkutano wa kumi kikao cha nane.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru Kawambwa (kulia) akiongea na James Mbatia (Kushoto)- katika viwanja vya Bunge leo. Baada ya Spika Anne Makinda(hayupo pichani) kutangaza rasmi Mitala ya Elimu inayotumika ni halali na ipo. (Pichani katikati) ni Charles Mwijage (Muleba Kaskazini)
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema akisoma Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa mwaka 2012 katika ukumbi wa Bunge leo
Mwenyekiti wa Bunge Mussa Zungu Azzan akifafanua kanuni mbalimbali Bungeni leo.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe(kushoto) akiongea na Joshua Nassari(Arumeru Mashariki) ndani ya ukumbi wa Bunge.
Picha zote n Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top