BULEMBO akikagua gati la kuegemeshea meli
linaloendelea kujengwa katika wilaya ya mafia. Gati hilo ambalo ni muhimu sana
kwa wananchi wa wilaya hiyo linatarajiwa kumalizika mwezi wa tatu mwaka huu.
Wengine katika picha ni viongozi wa CCM.
MWENYEKITI wa Jumuia ya Wazazi tanzania, Abdallah Bulembo akizungumza na Mkuu wa
kituo cha polisi cha wilaya ya Mafia kuhusu malalamiko ya askari wa usalama
barabarani wa kituo chake, aliyetajwa kwa jina moja la Luka kwamba amekuwa
akijihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa akimtaka afanye utaratibu
wa kumuhamisha katika kituo hicho ili kurudisha heshima ya jeshi hilo kwa
wananchi wa wilaya hiyo. Mkuu huyo wa kituo alimuahidi Bulembo kulifanyia kazi
suala hilo. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mafia Sauda Mtondoo.Picha na Mpiga
Picha Maalum
Post a Comment