Wadhamini wa Timu ya Taifa
(Taifa Stars), Kilimanjaro Premium lager, wamesema wanarishishwa na kiwango cha
timu hiyo kwa sasa huku wakiomba TFF iandae mechi nyingi za Staridi za kirafiki
hapa nyumbani.
Kauli hiyo imetolewa na
Meneja wa Bia ya Kilimanajro Premium Lager, George Kavishe siku moja baada ya
Stars kuicharaza Cameroon bao 1-0 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa katika
Uwanja wa Taimu hiiifa Jijini Dar es Salaam.
“Kwa kweli tunafurahishwa
na mafanikio ya timu hii tangu tuchukue udhamini mwezi Mei mwaka
jana….tumeiangalia ikicheza ndani na nje na kwa kweli kikosi ni kizuri kwani
kimewaletea watanzania ushindi,” alisema.
Aliwapongeza watanzania kwa
kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao kama kauli mbiu ya KIlimanajro
Premium Lager inavyosema…”Sherekea kilicho chetu.
“Hawa walikuwa wanajulikana
kama Simba wa Afrika lakini wameondoka wakiwa wamenyong’onyea baada ya kufungwa
1-0,” alisema.
Bw Kavishe alisema ushindi
huu wa Stars umewapa nafasi nzuri ya kuendelea kuidhamini Taifa Stars ili kuwapa
watanzania nafasi ya kusherekea kilicho chao kwa kupitia burudani ya
mpira.
“Dhidi watanzania
wanavyozidi kutuunga mkono kwa kunywa bia yetu ya Kilimanajro Premium Lager ndio
sisi tunazidi kupata fedha za kuidhamini timu na kuendelea kuwapa burudani ya
mpira,” alisema Kavishe.
Alisisitiza kuwa TFF
inatakiwa kuandaa mechi nyingi za kirafiki hapa nyumbani ili watanzania wazidi
kuiona timu yao ikicheza.
Huu ni ushindi mnono wa
pili mfululizo kwa timu ya Taifa baada ya kuichapa Zambia 1-0 Disemba mwaka
jana.
Kilimanjaro Premium Lager
imetoa udhamini wa zaidi ya Shilingi Bilioni 10 kwa miaka mitano. Huu ndio
udhamini mkubwa kabisa wa mpira ambao umewahi kutokea Tanzania.
Post a Comment