Meneja Mawasilianao wa
Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa (kushoto) akimkabidhi fedha kiasi cha shilingi
Milioni 5 mshindi wa Promosheni ya "MAHELA"Ofisa wa Polisi kanda maalumu ya
jijini Dar es Salaam Bi.Liberata Kaligita.Aliejishindia kwenye promosheni hiyo
inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,zaidi ya shilingi milioni 400 zinaendelea
kushindaniwa,katikati ni Ofisa Polisi Bethuel Sumari.
Meneja Mawasilianao wa
Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa (kushoto) akimsisitiza jambo mshindi wa
Promosheni ya"MAHELA"ambaeni dereva wa Bajaji Mbezi Kimara Bw.Paskal
Susuma(kulia)wakati wa kumkabidhi pesa zake kiasi cha shilingi Milioni 1
aliyojishindia katika promosheni hiyo inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,zaidi
ya shilingi milioni 400 zinaendelea kushindaniwa,katikati ni Meneja uhusiano wa
kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu.
*****
Promosheni ya MAHELA
inayoendeshwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, imeendelea
kusisimua hisia za watanzania kwa washindi zaidi kuendelea kupatikana na wakati
huu bahati ikiwaangukia Askari wa Jeshi la Polisi kanda maalumu Dar es Salaam
Bi.Liberata Kaligita na Dereva wa Bajaji ambae anaendesha bajaji za Mbezi
Kimara Bw.Paskal Susuma.
Akizungumza wakati wa droo
na makabidhiano ya pesa zao na Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania katika
makao Makuu ya kampuni hiyo yaliyoko Mlimani City jijini Dar es Salaam,Bi.
Liberata Kaligita ambae ni mkazi wa Galax Barabara ya Kilwa amesema kuwa mara
kadhaa alipokuwa akishiriki katika Promosheni hiyo Askari wenzake walimcheka
sana lakini leo hii wataamini kuwa Vodacom Tanzania kupitia promosheni yake hii
ya"MAHELA"hawana longolongo.
Kazi ni kwao kwa kujibu
maswali kwa ufasaa tu,Kwa upande wake Mshindi wa pili wa Milioni moja ambaye
amepatikana kutoka kwa washindi walioshiriki mara nyingi katika Promosheni hiyo
amesema kuwa kamwe hakukata tamaa kushiriki katika promosheni hiyo kwa kujua
kuwa ipo siku bahati itaangukia kwake na hakuweza kuizuia furaha yake kama
ilivyokuwa katika Mazungumzo na kuongeza kwa kusema kwasababu yeye ni dereva wa
bajaji anaipenda kazi yake lakini atafungua biashara ya M-pesa kwani Vodacom
imemwezesha kupitia promosheni hii ya MAHELA.
Post a Comment