Mheshimiwa Mathias Chikawe
(Mb), Waziri wa Katiba na Sheria leo amefungua Mkutano wa Jukwaa la Tume za
Uchaguzi za Nchi za SADC unaokutana Dar salaam kwa siku Mbili.
Jukwaa hilo linajumuisha
Tume za Uchaguzi kutoka nchi za Tanzania, Zambia, Botswana, Swaziland,
Madagascar, Angola, DRC, Lesotho, Malawi, Mauritius, Mozambique, Seychelles,
Zanzibar na Zimbabwe.
Jukwaa hilo lilianzishwa
mwaka 1998 kwa lengo ya kuleta chachu ya mabadiliko katika nchi za SADC kwenye
masuala ya uchaguzi. Jukwaa linahimiza uanzishwaji wa Tume huru za Uchaguzi,
umuhimu wa kuweka mazingira stahiki ya kisheria na kitaasisi ili kuziwezesha
Tume za Uchaguzi kufanya kazi za kusimamia uchaguzi kwa
ufanisi.
Mhe Chikawe pamoja na mambo
mengine amezitaka Tume za Uchaguzi zilizo katika Jukwaa hilo kuimarisha
ushirikiano wao kwa lengo la kuboresha chaguzi Barani Africa ili chaguzi hizo
ziwe kichocheo cha maendeleo na sio chanzo cha vurugu na vita.
Mhe. Chikawe amesema kwa
kupitia Jukwaa hilo, Tume za Uchaguzi zitaweza kutatua changamoto mbalimbali
zilizopo za kisheria, kimuundo, kitaalamu na kifedha zinazozikabili Tume nyingi
barani Africa ili kuhakikisha nchi za SADC zinakuwa na chaguzi huru na za
haki
Charles Joseph
Mmbando
LL.B (Mzumbe), LL.M - Human
Rights (Pretoria)
Private Secretary to the
Minister for Constitutional and Legal
Affairs
Mobile: + 255757020502
+255713477775
Post a Comment