Waziri wa Afya na Ustawi
wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi (hayupo pichani) akiwaongoza wageni waalikwa wakati akipokea magari mawili maalumu ya kusafirishia dawa. |
Mfanyakazi wa Bohari ya
Dawa (MSD), akionesha jinsi ya kubeba dawa ndani ya bohari hiyo kwa kutumia toroli maalumu. |
Dereva wa Bohari ya Dawa
(MSD), akionesha jinsi ya kubeba dawa ndani ya bohari hiyo kwa kutumia foku lifti. |
Waziri wa Afya na Ustawi
wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi (katikati), akiwa na viongozi mbalimbali kwenye hafla hiyo |
Wafanyakazi wa Bohari ya
Madawa (MSD), wakiwa kwenye hafla hiyo |
Na Dotto Mwaibale
RAIS Jakaya Kikwete ameiagiza Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii na Jeshi la Polisi
nchini kufanya msako na kuwafichua watu wote
watakaopatikana na dawa za Serikali
katika maduka binafsi.
Maagizo hayo ylitolewa na Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii kwa niaba ya Rais Kikwete
ambaye angekuwa mgeni rasmi kwenye
sherehe za
ufunguzi wa ghala la kisasa la
kuhifadhia dawa katika Makao Makuu ya Bohari ya
Dawa jijini Dar es Salaam leo.
"Natambua kuwa lipo tatizo la dawa na vifaa tiba vya serikali kupatikana katika maduka
ya dawa ya watu binafsi jambo ambalo linanikera sana nawaagizeni wachukukieni hatua
za kisheria wale wote watakao patikana na dawa hizo"
alisema Rais Kikwete.
Alisema Serikali haiwezi kuendelea kununua dawa
kwa dharama kubwa na zikaishia
katika mifuko ya watu wachache badala ya wananchi
walio wengi hususani wa vijijini.
Alisema Bohari ya dawa iliundwa mwaka 1994,
ikiwa nadira ya kufikisha dawa na vifaa
tiba karibu na wananchi ambapo tumeambiwa
kuwa
shughuli za MSD zimepanuka sana
hususani uwezo wa maghala umefikia mita za
mraba 51,800 na nusu ya hizo ni za
kukodisha kwa watu binafsi.
"Natambua kuwa gharama za ukodishaji wa magahala ni kubwa sana na ni vema MSD
ikawa na maeneo yake yenyewe bila kutegemea
maghala binafsi" alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete alizielekeza Halmashauri husika katika
kanda za MSD kuisaidia Bohari ya
dawa kupata maeneo mkakati ya uhifadhi wa dawa
na maeneo waliyonayo tayari
yaweze kupewa haki miliki.
Alisema chanjo ni hatua muhimu kwa ajili ya ya afya
za mama na mtoto ambapo mpango
wa taifa wa chanjo ulianza mwaka 1975 ukiwa unatoa
chanjo dhidi ya magonjwa kama
KifuaKikuu, Polia, Surua, Dondakoo, kifaduro na
Pepo Punda.
Alisema magonjwa mengine yaliyongezeka ni kinga
dhidi ya Homa ya Ini, Homa ua Uti
wa mgongo, nimonia na kinga dhidi ya magonjwa
ya kuhara.
Rais Kikwete aliongeza kuwa kinga ni haki ya kila
mtoto hivyo mahitaji ya chanajo
yamekuwa yanaongezeka kwaka hadi mwaka
kutokana na ongezeko la idadi ya watu.
"Ongezeko la idadi ya chanjo pamoja na ongezeko
la aina za chanjo imesababisha kuwa
na hitaji kubwa la maeneo ya kuhifadhi chanjo na kuzisambaza" alisema Kikwete.
Alisema Utunzaji wa chanjo unahitaji mfumo wa
mnyororo baridi hivyo kuhitaji vyumba
maalumu vyenye ubaridi, pamoja na gari lenye
vifaa vya kutunza ubaridi huo ili
kuhakikisha mnyororo baridi.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein
Mwinyi alisema ufunguzi wa gahala hilo
ni sehemu ya kutekeleza mpango mkakati wa MSD wa
kuhakikisha upatikanaji wa dawa
na vifaa tiba vyenye ubora unaokubalika na kwa
bei nafuu.
"Mpango huu umeandaliwa kwa kuzingatia Sera ya Afya ya kufikisha huduma bora za
afya kwa kila Mtanzania" alisema Mwinyi.
Alisema vyumba vya kuhifadhia chanjo na magari
maalumu ya kusafirishia chanjo
uliozinduliwa vitasaidia katika kutunza na
kusafirisha chanjo katika hali ya ubaridi kwa
mujibu wa miongozo ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ambayo Tanzania
inatekeleza.
Alisema ghala hilo linauwezo wa kuhifadhi
dawa na
vifaa tiba lina mita za mraba 4,280
na kuwa limejengwa kwa msaada wa Serikali ya
Marekani na Mfuko wa Dunia wa
Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu, Malaria na
limegharimu jumla ya Dola za Marekani
milioni 4 sawa na takribani sh.bilioni 6.4 za Kitanzania.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),
Cosmas Mwaifwani alisema ujenzi
wa ghala hilo ni matunda yaliyotokana na
safari za
Rais Kikwete nje ya nchi hususan
Marekani ambapo mei 2 mwaka 2009 akiwa katika
ziara nchini Marekani Rais wa nchi
hiyo Barack Obama aliahidi kuendelea kutoa
misaada katika maeneo mbalimbali
likiwemo la kuboresha huduma za kupambana na
maradhi ya Ukimwi kupitia shirika la
PEPFAR.
Alisema moja ya miradi inayoratibiwa na PEPFAR
ni ujenzi wa maghala makubwa katika
kanda za Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Tanga
na Tabora.
Mwaifwani alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais
Kikwete kwani matokeo ya juhudi zake
zimeleta matunda ambayo yanaonekana kwa Taifa.
Alisema ukamilishwaji wa miradi hiyo utaisaidia
Bohari ya Dawa kukomboa jumla ya
shilingi za Tanzania bilioni 1 katika mwaka
ujao wa
fedha ambazo wamekuwa wakilipa
kwa ajili ya kukodi maghala ya watu binafsi kwa ajili
ya kuhifadhi dawa, vifaa tiba na
vitendanishi kabla ya kusambazwa kwa walengwa.
Alisema Bohari ya Dawa imeendelea kutekeleza jukumu lake la msingi la kusambaza
dawa na vifaa tiba katika vituo vya afya hapa nchini
kwa niaba ya Serikali.
Aliongeza kuwa katika kutekeleza majukumu hayo
Bohari ya Dawa imefanikiwa
kufanikisha upatikanaji wa dawa ambapo imefikia
kati ya asilimia 70 hadi 75 ya mahitaji
dhidi ya asilimia 44 wakati Taasisi hiyo ilipo
anzishwa mwaka 1994.
Alisema mikoa 10 imeingizwa katika mfumo wa
kufikisha dawa moja kwa moja hadi
vituo vya afya na mikakati imewekwa ya kuingiza
mikoa yote ya Tanzania katika mfumo
huo kuanzia julai 2013 na kuwa mkakati huu
unazihusu pia hospitali za Wilaya, Mikoa na
Hospitali za Rufaa.
Mwaifwani alisema MSD imefungua mfumo
mpya
wa kisasa wa TEHAMA (EPICOR) ili
kurahisisha shughuli za usambaji ambao pia
umefadhiliwa na USAID
Post a Comment