Kamati ya Uchaguzi ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inawataarifu wananchi wote kwamba
baada ya kufanya usaili kwa waombaji uongozi wa TFF na Tanzania Premier League
Board (TPL Board), Kamati imefanya maamuzi yafuatayo:
1. TANZANIA PREMIER
LEAGUE BOARD
(a) Waombaji
uongozi wafuatao wamekidhi matakwa ya Kanuni za uendeshaji za TPL Board na
Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kamati inawatangaza kuwa wagombea wa
nafasi walizoomba kama ilivyoonyeshwa hapa chini:
NAFASI
INAYOGOMBEWA
|
S/N0.
|
JINA
|
MWENYEKITI
WA TPL BOARD
|
1.
|
Hamad
Yahya Juma
|
2.
|
Yusufali
Manji
| |
|
| |
MAKAMU
MWENYEKITI WA TPL BOARD
|
1.
|
Said
Muhammad Said Abeid (Kupitishwa kwake kutategemea matokeo ya uhakiki wa vyeti
vyake)
|
MJUMBE
–KAMATI YA UENDESHAJI (Management Committee)
|
1.
|
Kazimoto
Miraji Muzo
|
|
2.
|
Omary
Khatibu Mwindadi
|
(b) Mwombaji
uongozi Ndg. Christopher Peter Lunkombe hakukidhi matakwa ya Kanuni za
uendeshaji za TPL Board Ibara ya 28(2) kwa kuwa cheti chake cha Elimu ya
Sekondari kina utata. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imemwondoa kugombea nafasi ya
Mjumbe wa Kamati ya uendeshaji (Management Committee) ya TPL Board.
2. SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
(TFF)
(a) Waombaji
uongozi wafuatao wamekidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za
TFF.Kamati inawatangaza kuwa wagombea wa nafasi walizoomba kama
ilivyoonyeshwa hapa chini:
NAFASI
|
S/No.
|
JINA
|
RAIS
WA TFF
|
1.
|
Athumani
Jumanne Nyamlani
|
2.
|
Jamal
Emily Malinzi
| |
MAKAMU
WA RAIS WA TFF
|
|
|
2.
|
Ramadhan
Omar Nassib
| |
3.
|
Wallace
Karia
| |
MJUMBE
WA KAMATI YA
UTENDAJI
–
Kanda
ya 1 (Kagera, Geita)
|
|
|
1.
|
Kalilo
Samson
| |
2.
|
Salum
Hamis Umande Chama
| |
|
| |
Kanda
ya 2 (Mwanza, Mara)
|
1.
|
Jumbe
Oddessa Magati
|
2.
|
Mugisha
Galibona
| |
3.
|
Samwel
Nyalla
| |
4.
|
Vedastus
F.K Lufano
| |
|
| |
Kanda
ya 3 (Shinyanga, Simiyu)
|
1.
|
Epaphra
Swai
|
|
| |
Kanda
ya 4 (Arusha, Manyara)
|
|
|
1.
|
Elley
Simon Mbise
| |
2.
|
Omar
Walii Ali
| |
|
| |
Kanda
ya 5 (Tabora, Kigoma)
|
1.
|
Ahmed
Idd Mgoyi
|
2.
|
Yusuf
Hamis Kitumbo
| |
|
| |
Kanda
ya 6 (Rukwa, Katavi)
|
|
|
1.
|
Blassy
Mghube Kiondo
| |
2.
|
Seleman
Bandiho Kameya (Kupitishwa kwake kutategemea matokeo ya uhakiki wa vyeti
vyake)
| |
|
| |
Kanda
ya 7 (Iringa, Mbeya)
|
1.
|
David
Samson Lugenge
|
2.
|
John
Exavery M. Kiteve
| |
3.
|
Lusekelo
E. Mwanjala
| |
|
| |
Kanda
ya 8 (Ruvuma, Njombe)
|
1.
|
James
Patrick Mhagama
|
2.
|
Stanley W.
D Lugenge
| |
|
| |
Kanda
ya 9 (Mtwara, Lindi)
|
1.
|
Athuman
Kingome Kambi
|
2.
|
Francis
Kumba Ndulane
| |
3.
|
Zafarani
Mzee Damoder
| |
|
| |
Kanda
ya 10 (Dodoma, Singida)
|
1.
|
Hussein
Zuberi Mwamba
|
2.
|
Stewart
Ernest Masima
| |
|
| |
Kanda
ya 11 (Morogoro, Pwani)
|
|
|
1.
|
Riziki
Juma Majala
| |
2.
|
Twahil
Twaha Njoki
| |
|
| |
Kanda
ya 12 (Kilimanjaro, Tanga)
|
1.
|
Davis Elisa
Mosha
|
2.
|
Khalid
Abdallah Mohamed
| |
3.
|
Kusianga
Mohamed Kiata
| |
|
| |
Kanda
ya 13 (Dar es salaam)
|
1.
|
Alex
Crispine Kamuzelya
|
2.
|
Juma
Abbas Pinto
| |
3.
|
Muhsin
Said Balhabou
|
(b) Waombaji
uongozi wafuatao hawakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za
TFF. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imewaondoa kugombea nafasi walizoomba kama ilivyoonyeshwa hapa chini:
(i) Ndg. Omary Mussa
Nkwarulo anayeonba kugombea nafasi ya Rais wa TFF hakukidhi matakwa
ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na
ufahamu wa kuridhisha kuhusu majukumu na wajibu wa nafasi anayoomba na uwezo wa
kutekeleza majukumu na malengo ya TFF.
(ii) Ndg. Michael Richard
Wambura anayeonba kugombea nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF hakukidhi
matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kuwa Ndg.
Michael Wambura alifungua kesi ya madai namba 100 ya 2010 kwenye Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam dhidi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba akiwa
ni mwanachama wa Klabu ya Simba, kinyume na Katiba ya Klabu ya Simba. Kwa
kufanya hivyo, Ndg. Michael Wambura alivunja Katiba ya Klabu ya Simba, alikiuka
Katiba ya TFF na Katiba ya FIFA.
(iii) Pia Kamati inaheshimu maamuzi
yaliyotolewa na Kamati ya Rufaa ya TFF kuhusu uchaguzi mwaka 2008 kwamba Bw.
Michael R. Wambura hakukidhi matakwa ya Ibara ya 29(7) ya Katiba ya TFF na Ibara
ya 9 ya Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kwa mujibu wa Katiba ya TFF na Kanuni za
Uchaguzi za TFF, Kamati ya Uchaguzi ya TFF haina mamlaka ya kubadilisha maamuzi
yaliyofikiwa na Kamati hiyo ya Rufaa. Maamuzi hayo yanaweza tu kubadilishwa na
Mahakama ya usuluhishi wa masuala ya michezo (CAS).
(iv) Ndg. Abdallah Hussein
Musa anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda
Na. 1 (Kagera, Geita) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za
Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu
majukumu na wajibu wa nafasi anayoomba na uwezo wa kutekeleza majukumu na
malengo ya TFF.
(v) Ndg. Mbasha
Matutu anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia
Kanda Na. 3 (Shinyanga, Simiyu) hakukidhi matakwa ya Katiba ya
TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa aliingilia mchakato wa
Uchaguzi kwa kushirikiana na waweka pingamizi dhidi ya mgombea
mwenzake.
(vi) Ndg. Charles
Mugondo anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia
Kanda Na. 4 (Arusha, Manyara) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF
na Kanuni za Uchaguzi za TFF kwa kuwa vyeti vyake vya Elimu ya Sekondari na
cheti cha Ualimu vina utata.
(vii) Ndg. Ayubu
Nyaulingo anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia
Kanda Na. 6 (Rukwa, Katavi) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF
na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 3 inayotaka awe na uzoefu wa uendeshaji
wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5) na pia hakukidhi
Ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu majukumu na wajibu wa
nafasi anayoomba na uwezo wa kutekeleza majukumu na malengo ya TFF.
(viii) Ndg. Nazarius A.M
Kilungeja anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia
Kanda Na. 6 (Rukwa, Katavi) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF
na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa amekuwa sehemu ya migogoro
ya muda mrefu mkoani Rukwa.
(ix) Ndg. Eliud Peter
Mvella anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia
Kanda Na. 7 (Iringa, Mbeya) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF
na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa si mwaminifu kwa kukiuka
uamuzi wa pamoja wa Kamati ya Utendaji ya TFF kuhusu mabadiliko ya
Katiba.
(x) Ndg. Farid
Nahdi anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia
Kanda Na. 11 (Morogoro, Pwani) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF
na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(2) na (7) kwa kuwa maelezo ya umri wake
na vyeti vya elimu havikubaliani.
(xi) Ndg. Hassan Othuman Hassan
anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na.
11 (Morogoro, Pwani) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara
ya 11(5) kwa kuwa hakuhudhuria usaili.
(xii) Ndg. Omary Isack
Abdulkadir anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia
Kanda Na. 13 (Dar es salaam) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za
TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa alikaidi maagizo ya TFF ya kuahirisha uchaguzi wa
chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) na maagizo ya TFF kwa kuwa
alienguliwa kwenye mchakato wa uchaguzi wa FRAT kwa kutotimiza matakwa ya Kanuni
za uchaguzi za wanachama wa TFF.
(xiii) Ndg. Shafii Kajuna
Dauda anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia
Kanda Na. 13 (Dar es salaam) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za
TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa si mkweli: aliposhindwa kwenye uchaguzi wa Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam (DRFA) alipotosha umma kuhusu ushiriki wake
kwenye uchaguzi huo na mchakato mzima wa uchaguzi. Pia hana ufahamu kuhusu
Katiba ya TFF na majukumu ya Kamati ya Utendaji ya TFF.
3. Usaili uliofanyika kwa waombaji uongozi ulizingatia pia taarifa
zilizoifikia Kamati ya Uchaguzi ya TFF kupitia pingamizi zilizowasilishwa dhidi
ya waombaji uongozi wa TFF na TPL Board.
4. Uchaguzi wa TPL Board utafanyika tarehe 22 Februari 2013, na Uchaguzi
wa TFF utafanyika tarehe 24 Februari 2013 jijini Dar es salaam.
Post a Comment