TUME Huru ya Uchaguzi Kenya (IEBC) imemthibitisha mgombea wa urais, Uhuru Kenyatta kuwa mgombea rasmi wa kiti hicho.
Mwenyekiti wa tume hiyo huru nchini humo, Isaack Hassan alikubali vielelezo vilivyowasilishwa kwake kuhusu mgombea huyo na kumpitisha rasmi.
Baada ya kupitishwa kwake huko Kenyatta alisema kwamba Jubilee imesimama kwa ajili ya kutetea haki za wananchi wa Kenya.
Alisema wanachokifanya sasa ni kuhakikisha masuala ya uchaguzi yanaenda salama nchini humo.
“Tumeshajizatiti na tumeahidi kutoa ushirikiano kwa wananchi wetu hivyo ninachowaomba ni kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kupiga kura,” alisema.
Alisema kwamba kwa sasa hivi Wakenya wanatakiwa kufahamu ni nani hasa kiongozi wa kumchagua ambaye anaweza kuwasaidia katika masuala ya maendeleo. Alisema kwa kuwataka wananchi wa Kenya kuacha kuogopa kupiga kura.
“Msiogope kujitokeza kupiga kura kwa wingi wananchi wa Kenya kumchagua mnayemtaka,” alisema.
MWANANCHI
MWANANCHI
Post a Comment