Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

VIJANA WATAKIWA KUWA WABUNIFU WA MIRADI ENDELEVU


images
HEKA PAUL- MAELEZO
VIJANA nchini wameshauriwa kutumia fedha za mikopo wanazozipata kwa ajili ya kuanzisha biashara endelevu zitakazowasaidia kujikwamua kimaisha na kujiletea maendeleao.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana nchini Profesa Elisante Ole Gabriel kutoka Wizara ya Habari ,Vijana,Utamaduni na Michezo wakati akitoa elimu kwa vijana wajasiliamali wa manispaa ya Kinondoni ,Temeke na Ilala ,jijini Dares Salaam ikiwa ni ziara yakr ya muda wa siku mbili iliyoanza leo
Alisema vijana yoyote ambaye ni mjasiriamali anatakiwa kuwa na uwezo na uwelewa wa kuendesha mradi huo pamoja na kuzitambua changamoto atakazokumbana nazo wakati shughuli zake.

Profesa Gabriel alisema kuwa ni muhimu kwa kila mjasiriamali kijana anaetaka kuanzisha mradi kufanya biashara halali ambayo inakibali na pamoja na kujua namna ya kupanga bei ya biashara zake.
Aliongeza kuwa ipo mihimili mitatu ya maendeleo ya biashara ambayo vijana wenyewe, serikali ambayo inatakiwa kuweka mfumo mzuri kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya vijana pamoja na kuwepo kwa wadau wengine wa maendeleo.
Profesa huyo alizitaja gharama tatu za msingi katika kuanzishia mradi ambazo ni lazima kuwepo na malighafi, watumishi na uangalizi wa mradi huo.
Aliwataka vijana pia kuepuka kubaguliwa au kubaguana kwa kupitia mlango wa siasa, dini na kikabila wanapoendesha shughuli zao za ujasiriamali.
Naye Afisa Biashara wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Ananias Kamundo alisema kuwa ni muhimu kwa kila mjasiriamali mwenye biashara yoyote ambayo ni halali kuifungulia leseni ambayo mjasiriamali malipo na lazima awe na namba ya mlipa kodi ambayo ataipata Mamlaka ya Mapato nchini (TRA)pamoja na kitambulisho kitakacho mtambulisha kuwa ni raia wa nchini.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top