Mtela Mwampamba |
KILIO CHA USALITI – PART TWO.
Wakati
mwingine tunajikuta tunalazimika kuyasema hata yale ambayo hatukupanga wala
kufikiria kuyasema.,nimekuwa nikipigiwa simu na ndugu zangu na rafiki zangu
ambao bado wako chadema wakiniuliza kwanini nimeamua kuyasema ninayoyasema, tena
kwa lugha kama hii (inayobainisha), nami nimekuwa nikiwajibu kuwa "hivi haiwi
faraja kwenu kuwa yupo mmoja aliyewahi kuwa mfano wenu anayetaka kuwaokoa na
hatari yenye kuangamiza..?
Nadhani wengi katika wao wamenielewa lakini
nitazidi kuwaeleweshaa wale ambao bado wanaubutu na kutu imejaa katika fikra na
mitazamo yao.
Nimeeleza juu ya kukanwa na usaliti uliofanywa kwa LuDOVICK
na nikaishia hapo, nikidhani kuwa itakuwa imetosha kuwafungua mawazo na
kuwasaidia vigezo na vipambanuzi vya kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi, maamuzi
huru ambayo yatatokana na fikra zinazojitawala za kila mmoja katika upekee wake,
si fikra za mkumbo (mob psychology) wala si fikra mgando na zilizosinyaa
(dormant and dead reasoning), lakini nitawaongeza na hili la leo kuyaamsha
mawazo hayo yaliyoganda na kuwafanya muishi kwa Uhai wa fikra
Huru.
Napenda nianze kwa kuwaambia kuwa si mara ya kwanza kwa viongozi wa
Chadema kuwakana wapambanaji wao na vijana waliokuwa wanajitolea hali na mali,
wanajitolea nafsi na uhai kuipigania Chadema. Nitawaambieni juu ya wachache
waliowahi kusalitiwa na kukanwa hadharani na vongozi waandamizi wa chadema kama
ifuatavyo:-
i) DEUS MALLYA:
Kwa mara ya kwanza nakutana na DEUS
ilikuwa ni mwaka 2007, nikiwa nimejiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam, ambapo
nilishakuwa mwanachadema kabla ya kuingia Chuo Kikuu, hivyo nilipofika chuo
nilijaribu na kufanikiwa kukutana na vijana wapambanaji wa Chadema hasa wale
waliokuwa wanatumikia Makao Makuu ndipo nilipokutana na DEUS MALLYA ambae
alikuwa akitumika katika kuchapisha mabango na vipeperushi ambavyo vilikuwa
vinabeba ujumbe wa Chadema na falsafa mbalimbali za Ukombozi ambazo chadema
ilikuwa ikinajinasbisha nazo.
Nilipokutana na DEUS tulipanga na kupeana
ushauri wa jinsi ya kueneza na kusambaza vipeperushi hivyo na hatimae
aliniunganisha na JOHN MNYIKA ambae kwa kipindi hicho alikuwa ni Mkurugenzi wa
Vijana na Afisa wake akiwa Marehemu Regia Mtema, ambapo DEUS alikuwa ni mtu wa
karibu na maafisa hao, hasa MNYIKA.
Na walikuwa pamoja na kufanya mambo
mengi, ninayoyakumbuka ni pamoja na;
a) Safari ya DEUS mallya kuelekea
LIBYA katika kongamano la vijana akiwa muwakilishi wa vijana kutoka chadema chini
ya usimamizi wa Mnyika.
b) Safari ya RUSSIA ambapo DEUS alinieleza kuwa
alienda kwa mafunzo maalum.
Lakini Mnamo mwezi wa tisa (9) mwaka 2008,
baada ya kutokea kwa kifo cha kutatanisha cha Mheshimiwa CHACHA WANGWE ambapo
DEUS alikuwa ni Dereva na mshukiwa wa kwanza katika ajali ile, JOHN MNYIKA
alimkana DEUS mara mbili, mara ya kwanza ni pale apohojiwa na maafisa wa polisi
juu ya kijana DEUS akamkana, na mara ya pili alipokutana na vyombo vya habari
kuzungumzia sakata hilo akamkana kwa mara ya pili.
Hata baada ya kesi ya
DEUS kumalizika na kisha DEUS kuachiwa huru, nilizungumza na DEUS juu ya kukanwa
na MNYIKA na DEUS alinijibu kuwa mshikaji alimuomba radhi na kumtaka asahau
yaliyopita na DEUS alikiri kumsamehe na imebaki hivyo mpaka hivi sasa (hili
anaweza kulithibitisha DEUS MALLYA mwenyewe kwakuwa yu-hai)
Lakini
haikuishia kwa MNYIKA pekee bali hata BENSON KIGAILA ambae ni Mkurugenzi wa
Oganaizesheni na Mafunzo aliwahi kumkana na anaendelea kumkana mpaka leo hii,
kiasi kwamba DEUS akienda pale Makao Makuu na akikutana na BENSON huwa
anamuambia kuwa asiwe anakuja Makao Makuu maana Chama kitachafuka kwa kuonekana
MALLYA pale.
Ni mtu ambae hafikiri sawasawa tu ndie atakayeweza kusema
USALITI huu hauna asili ya ndani na kuwa ni hulka za viongozi wakuu wa Chadema
kuendelea asili yao hiyo.
ANGALIZO:
Nitasema kama nilivyokutangulia
kusema hapo awali juu ya hatma ya vijana ndani ya chadema, na leo nitasema
hivi;
IKIWA HII MITI MIBICHI INATENDEWA HIVI., JE NINYI MITI MIKAVU
MTATENDEWA VIPI..? ambao hata makao makuu ya Chama hamyajui wala hakuna
anayewajua zaidi ya kuwatumia kwenye maandamano na mikakati yao.
Wakati mwingine tunajikuta tunalazimika kuyasema hata yale ambayo hatukupanga wala kufikiria kuyasema.,nimekuwa nikipigiwa simu na ndugu zangu na rafiki zangu ambao bado wako chadema wakiniuliza kwanini nimeamua kuyasema ninayoyasema, tena kwa lugha kama hii (inayobainisha), nami nimekuwa nikiwajibu kuwa "hivi haiwi faraja kwenu kuwa yupo mmoja aliyewahi kuwa mfano wenu anayetaka kuwaokoa na hatari yenye kuangamiza..?
Nadhani wengi katika wao wamenielewa lakini nitazidi kuwaeleweshaa wale ambao bado wanaubutu na kutu imejaa katika fikra na mitazamo yao.
Nimeeleza juu ya kukanwa na usaliti uliofanywa kwa LuDOVICK na nikaishia hapo, nikidhani kuwa itakuwa imetosha kuwafungua mawazo na kuwasaidia vigezo na vipambanuzi vya kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi, maamuzi huru ambayo yatatokana na fikra zinazojitawala za kila mmoja katika upekee wake, si fikra za mkumbo (mob psychology) wala si fikra mgando na zilizosinyaa (dormant and dead reasoning), lakini nitawaongeza na hili la leo kuyaamsha mawazo hayo yaliyoganda na kuwafanya muishi kwa Uhai wa fikra Huru.
Napenda nianze kwa kuwaambia kuwa si mara ya kwanza kwa viongozi wa Chadema kuwakana wapambanaji wao na vijana waliokuwa wanajitolea hali na mali, wanajitolea nafsi na uhai kuipigania Chadema. Nitawaambieni juu ya wachache waliowahi kusalitiwa na kukanwa hadharani na vongozi waandamizi wa chadema kama ifuatavyo:-
i) DEUS MALLYA:
Kwa mara ya kwanza nakutana na DEUS ilikuwa ni mwaka 2007, nikiwa nimejiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam, ambapo nilishakuwa mwanachadema kabla ya kuingia Chuo Kikuu, hivyo nilipofika chuo nilijaribu na kufanikiwa kukutana na vijana wapambanaji wa Chadema hasa wale waliokuwa wanatumikia Makao Makuu ndipo nilipokutana na DEUS MALLYA ambae alikuwa akitumika katika kuchapisha mabango na vipeperushi ambavyo vilikuwa vinabeba ujumbe wa Chadema na falsafa mbalimbali za Ukombozi ambazo chadema ilikuwa ikinajinasbisha nazo.
Nilipokutana na DEUS tulipanga na kupeana ushauri wa jinsi ya kueneza na kusambaza vipeperushi hivyo na hatimae aliniunganisha na JOHN MNYIKA ambae kwa kipindi hicho alikuwa ni Mkurugenzi wa Vijana na Afisa wake akiwa Marehemu Regia Mtema, ambapo DEUS alikuwa ni mtu wa karibu na maafisa hao, hasa MNYIKA.
Na walikuwa pamoja na kufanya mambo mengi, ninayoyakumbuka ni pamoja na;
a) Safari ya DEUS mallya kuelekea LIBYA katika kongamano la vijana akiwa muwakilishi wa vijana kutoka chadema chini ya usimamizi wa Mnyika.
b) Safari ya RUSSIA ambapo DEUS alinieleza kuwa alienda kwa mafunzo maalum.
Lakini Mnamo mwezi wa tisa (9) mwaka 2008, baada ya kutokea kwa kifo cha kutatanisha cha Mheshimiwa CHACHA WANGWE ambapo DEUS alikuwa ni Dereva na mshukiwa wa kwanza katika ajali ile, JOHN MNYIKA alimkana DEUS mara mbili, mara ya kwanza ni pale apohojiwa na maafisa wa polisi juu ya kijana DEUS akamkana, na mara ya pili alipokutana na vyombo vya habari kuzungumzia sakata hilo akamkana kwa mara ya pili.
Hata baada ya kesi ya DEUS kumalizika na kisha DEUS kuachiwa huru, nilizungumza na DEUS juu ya kukanwa na MNYIKA na DEUS alinijibu kuwa mshikaji alimuomba radhi na kumtaka asahau yaliyopita na DEUS alikiri kumsamehe na imebaki hivyo mpaka hivi sasa (hili anaweza kulithibitisha DEUS MALLYA mwenyewe kwakuwa yu-hai)
Lakini haikuishia kwa MNYIKA pekee bali hata BENSON KIGAILA ambae ni Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo aliwahi kumkana na anaendelea kumkana mpaka leo hii, kiasi kwamba DEUS akienda pale Makao Makuu na akikutana na BENSON huwa anamuambia kuwa asiwe anakuja Makao Makuu maana Chama kitachafuka kwa kuonekana MALLYA pale.
Ni mtu ambae hafikiri sawasawa tu ndie atakayeweza kusema USALITI huu hauna asili ya ndani na kuwa ni hulka za viongozi wakuu wa Chadema kuendelea asili yao hiyo.
ANGALIZO:
Nitasema kama nilivyokutangulia kusema hapo awali juu ya hatma ya vijana ndani ya chadema, na leo nitasema hivi;
IKIWA HII MITI MIBICHI INATENDEWA HIVI., JE NINYI MITI MIKAVU MTATENDEWA VIPI..? ambao hata makao makuu ya Chama hamyajui wala hakuna anayewajua zaidi ya kuwatumia kwenye maandamano na mikakati yao.
on Thursday, March 21, 2013
Post a Comment