Watafiti
na wanasayansi nchini Tanzania wametakiwa kufanya tafiti za kiungunduzi ambazo
zitaleta manufaa na kusaidia jamaii ya watanzania
.
Hayo
yamesema na leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dr. Mwele Malecela(pichani juu) wakati wa semina ya siku moja ya wagunduzi mbalimbali
iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya NIMR na Shirika la Grand Challenges la nchini
Canada.
Dkt. Malecela amesema umefika wakati sasa kwa wagunduzi mbalimbali wa
Kitanzania kuanza kungundua njia mbalimbali za kuweza kutatua matatizo yaliyopo
katika jamii hasa katika sekta ya
afya.
Semina hiyo ya siku moja ilikuwa na lengo la kuhamasisha wangunduzi
sekta ya afya ambapo baadhi ya wanasayansi wagunduzi kadhaa walitoa taarifa zao
za awali za namna ya kukabiliana na matizo kadha hasa kwa Mama na
mtoto.
Wagunduzi kadhaa waliweza kuzungumzia gunduzi zao katika semina hiyo
na miongini mwa hizo ni pamoja na ile ya hali ya Utapiamlo unaofanywa na Dkt.
Magreth Kagashe kutoka Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Bianadamu Ifakara
ambayo inafanyika katika Vijiji vya
Kilombero.
Ugunduzi mwingine ni wa namna ya kusafisha maji na kuyaweka katika
hali salama kupitia njia ya Takasa maji, na kuyaweka taika hali salama nay a
usafiugunduzi unaofanya na Kijakazi Mashoto na Ugunduzi mwingine ni matumizi ya
Maua ya Rosella katika kukabiliana na Upungufu wa damu kwa mama na
mtoto.
Dkt. Malecela amesema ya kuwa ugunduzi unaofanyika sasa na kupewa
fedha na Grand Challenge ya Canada unatakiwa uwe ugunduzi ambao utaleta
mabadiliko na kubadili maisha ya
wananchi.
“Mara nyingi wanasayansi wamekuwa wakifanya tafiti mbalimbali na
kugundua matatizo mengi katika jamii lakini mara chache watafiti hawa wametafuta
suluhisho ya hayo matatizo au magonjwa katika jamii hizo ...kwahiyo hivi sasa
wanasayansi wagunduzi wa kitanzania umefikia hatua ya kugundua vitu ambavyo
vitasaidia jamii,” alisema
Dkt.Malecela.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Grand Challenge Canada, Peter Singer
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya semina hiyo iliyofanyika Makao
Makuu ya NIMR jijini Dar es Salaam
leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya
Binadamu (NIMR) Dr. Mwele Malecela
akipiga picha na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Grand Challenge Canada, Peter Singer mara baada ya kuzungumza
na waandishi wa habari Makao Makuu ya NIMR jijini Dar es Salaam
leo.
Wanasayansi wagunduzi mbalimbali wakifuatilia kwa makini mazungumzo
ya wagunduzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya
Binadamu (NIMR) Dr. Mwele Malecela na Afisa Mtendaji
Mkuu wa Grand Challenge Canada, Peter Singer wakifuatilia kwa ukaribu mazungumzo
ya Wagunduzi wa Kitanzania katika Sejmina ya siku moja iliyofanyika NIMR jijini
Dar es Salaam leo.
Mwanasayansi Mkunduzi wa kitanzania kutoka Taasisi ya utafiti wa
Magonjwa Ifakara, Dkt. Magreth Kagashe akiwasilisha taarifa yake ya ugunduzi juu
ya hali ya utapiamlo na namna ya kukabiliana nao katika jamii na kuokoa vifo vya
watoto chini ya miaka 5 Kilombero.
Mwanasayansi Mkunduzi wa kitanzania kutoka Emmanuel Peter
akiwasilisha taarifa yake ya ugunduzi juu ya matuzimi ya unga wa uzalishaji wa
unga wa Maua ya Rosella katika kukabiliana na upungu wa damu kwa akina mama
wajawazito na watoto.
Prof. Esther Mwaikambo ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto
kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Herbert Kairuku (HKMU) akiulizwa swali. Kulia ni
Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
ambaye pia ni Mtafiti Mkuu Kiongozi, Dk. Leonard Mboera kutoka Taasisi ya Taifa
ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).
Prof. Esther Mwaikambo ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto
kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Herbert Kairuku (HKMU) akichangia
mada.
Wanasayansi wagunduzi mbalimbali wakifuatilia kwa makini mazungumzo
ya wagunduzi. Hii ni mara ya tatu sasa kwa Wagunduzi wa kitanzania kupata fedha
za kuendesha kugunzi zao nah ii ndio iliyo na manufaa zaidi kuliko zote.
credits: Father Kidevu
Post a Comment